Prof. Mwamfupe apongeza wadau wa elimu
Na. John Masanja , MIYUJI Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe awapongeza wadau wa elimu kwa jitihada zao kwenye kukuza sekta ya elimu na kuchangia ufaulu wa wanafunzi. Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe Pongezi hizo alizitoa kwa walimu, wazazi na wadau mbalimbali wa elimu kwa ushirikiano mzuri katika kukuza na kuinua sekta ya elimu ndani ya Jiji la Dodoma kwenye kikao cha wadau wa elimu na utoaji tuzo za kitaaluma kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi St. Gasper jijini Dodoma. “Natambua sana kuna changamoto nyingi ambazo mnakutana nazo wakati wa utendaji kazi wenu lakini hamjawahi kutuangusha na haya mafanikio tunayoyaona sasa hivi katika elimu ni matunda ya uwekezaji wa pamoja” alisema Prof. Mwamfupe. Vilevile, alipendekeza kufanyika kwa vikao vya wadau wa elimu kuanzia ngazi za chini ambako watu wengi hufikiwa katika kutoa ushauri na kuona namna gani mawazo yao yatakuwa na manufaa katika kuleta mab...