Kata ya Mkonze yaanza mafunzo ya 10% kwa vikundi
Na. Dennis Gondwe, KATA ya Mkonze imeanza kutoa mafunzo kuhusu mikopo ya asilimia 10 inayotolewa bila riba na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwajengea uelewa wa uwepo wa mikopo hiyo na taratibu za kuipata. Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Mkonze, Theresia Camilius wakati akitoa mafunzo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Mkonze, Theresia Camilius wakati akitoa mafunzo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Shule ya Msingi Mkonze iliyopo Kata ya Mkonze Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Theresia alisema kuwa mafunzo hayo yanahusisha vikundi vilivyosajiliwa na vinavyotarajia kuomba mkopo, vikundi ambavyo havijasajiliwa na vinatarajia kuomba mkopo ili viweze kufahamu mchakato na kufanya usajili na kuomba mikopo ya asilimia 10. “Matarajio ya mafunzo haya ni walengwa na wanufaika wa mikopo hii waweze kuelewa fedha zina...