Maadhimisho ya Siku ya Kichaa cha Mbwa kutoa elimu kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha Mbwa
Na. Asteria Frank, DODOMA Maadhimisho ya siku ya kichaa cha mbwa duniani yanalenga kuelimisha jamii juu ya kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha mbwa pamoja na kutowa chanjo kwa paka na mbwa ili kuwakinga na ugonjwa huo. Maadhimisho hayo yamefanyika katika ofisi za kituo za huduma za mifugo kanda ya kati Dodoma mjini ambapo wamefahamisha kuhusu kichaa cha Mbwa Pamoja na kutoa chanjo, dawa ya kuzuia viroboto na dawa za Minyoo kwa Mbwa na Paka. Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Hussein Nyenye katika maadhimishi ya siku ya kichaa cha mbwa duniani yaliyofanyika katika Kituo cha Huduma za Mifugo Kanda ya Kati, kilichopo jijini Dodoma. Nyenye alisema kuwa ni muhimu kwa wafugaji wa mbwa na paka kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kuweza kuwapatia mbwa na paka chanjo kwa wakati sahihi kuzuia magojwa mbalimbali kwa wanyama hao na wafugaji wenyewe. Alisema kuwa shughuli ya kudhibiti kichaa cha mbwa haiwezakani kufanyika na watu wa mifugo...