Posts

Showing posts from May 2, 2026

MIL. 544,335,626 ZAJENGA SHULE YA SEKONDARI MICHESE

Na. Dennis Gondwe, MKONZE SHILINGI 544,335,626 zimekamilisha ujenzi wa Shule ya Sekondari Michese na kuwawezesha wanafunzi 555 kupata elimu ya sekondari karibu na maeneo wanayoishi na kuwaondolea kero ya kutembea umbari mrefu kufuata elimu. Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa akisoma taarifa ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Michese kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI iliyotembelea na kukagua ujenzi wa shule hiyo. Fungo alisema “k iasi cha fedha kilichotolewa kwa ajili ya ujenzi ni shilingi 544,225,626 chanzo cha fedha kikiwa ni SEQUIP. Fedha zilipokelewa Mwezi Oktoba, 2023 na ujenzi ulianza rasmi Mwezi Novemba, 2023 na kukamilika Mwezi Mei, mwaka 2024. Utaratibu wa ujenzi uliotumika ni force akaunti na mradi ulikamilíka kwa wakati na shule ilianza rasmi mwaka 2024 na kusajiliwa kwa jina la Michese Sekondari, Namba ya usajili S.6625”. Alisema kuwa u jenzi wa shule hiyo ulifanyika kwa awamu tatu, awamu ya kw...

JIJI LATEKELEZA MKAKATI WA KUBORESHA MAENEO YA WAZI

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inatekeleza mkakati wa uboreshaji maeneo ya wazi kwa kusimamia udhibiti na usimamizi wa sheria na kufanya uondoaji wa maendelezo ya kudumu yaliyokiuka masharti na kuboresha miundombinu ya maeneo ya michezo. Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa akisoma taarifa ya uboreshaji wa maeneo ya wazi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) iliyofanya ziara katika jiji hilo. Fungo alisema kuwa halmashauri ilifanya zoezi la mapitio ya hali ya maeneo ya wazi ili kubaini kama yanatumika kwa mujibu wa sheria. “Halmashauri inatekeleza mkakati wa u dhibiti na usimamizi wa sheria katika maeneo ya wazi, zoezi la uondoaji wa maendelezo ya kudumu yaliyokiuka masharti ya uendelezaji limefanyika katika eneo la wazi lililopo Majengo maarufu kama kwa Kato, eneo la Rose Garden na maeneo mengine 47 ambayo tayari wame...

JIJI LA DODOMA LATUMIA MIL. 23 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetumia zaidi ya shilingi milioni 23 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo fedha kutoka serikali kuu, mapato ya ndani na wahisani pamoja na bakaa. Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa akiwasilisha taarifa fupi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Alisema kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai, 2025 hadi kufikia Machi, 2026 halmashauri imetumia jumla ya shilingi 23,815,713,415.02 sawa na asilimia 91.19 ya fedha zilizopokelewa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. “Kati ya fedha hizo, shilingi 6,406,582,002.56 ni fedha kutoka serikali kuu, shilingi 16,807,859,627.46 mapato ya ndani, shilingi 601,771,785.00 fedha za wahisani na shilingi 5,279,467,344.52 ni fedha za bakaa. Kwa kipindi cha kuanzia Julai, 2025 hadi kufikia Machi, 2026, hal...