Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Atembelea Maonesho ya Nanenane 2025 Jijini Dodoma
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Salim Msangi, atembelea banda la TCAA pamoja na mabanda mengine kadhaa katika Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma. Ziara hii ililenga kuonyesha huduma zinazotolewa na TCAA na kuhamasisha umma kuhusu masuala ya usafiri wa anga. Katika ziara hiyo, Msangi alionesha kuridhishwa na namna TCAA inavyotoa huduma na elimu kwa wananchi, hasa kuhusu usalama wa anga, matumizi salama ya ndege zisizo na rubani (ndege nyuki), na fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya usafiri wa anga. Alieleza kuwa huduma zinazotolewa na TCAA zinachangia pakubwa katika kuimarisha usalama na maendeleo ya sekta hiyo. Vilevile, alifurahishwa na ushirikiano wa watumishi wa TCAA katika kuelimisha umma, akiwapongeza kwa kujituma na kuendelea kutoa taarifa muhimu kwa wananchi kuhusu masuala ya usafiri wa anga. Alisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana na wadau wengine katik...