Walimu wakuu Jiji la Dodoma kupatiwa Mafunzo ya NeST
Na. Faraja Mbise, DODOMA Walimu wakuu kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamepatiwa mafunzo juu ya ununuzi kwa njia ya mtandao serikalini yatakayoboresha utendaji kazi na kuwawezesha kupata mafundi na watoa huduma kupitia mfumo wa ununuzi ‘ National e-Procurement System of Tanzania’ yaani ‘NeST’. Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Vincent Odero akifungua Mafunzo ya Ununuzi kwa njia ya Mtandao (NeST) Mafunzo hayo yameanza leo tarehe 21 Januari, 2025 na Kitengo cha Ununuzi na Ugavi cha Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kwa walimu wakuu wa shule za msingi katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Umonga. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Vincent Odero alisema kuwa mfumo wa manunuzi serikalini kwa njia ya kielektroniki ni mfumo mzuri na umerahisisha mchakato mzima wa manunuzi na umeleta ufanisi mkubwa katika ununuzi wa umma katika maeneo mbalimbali. “Mfumo huu ni mzuri, umerahisisha ...