Posts

Showing posts from April 2, 2025

Kata ya Ipala ipo mstari wa mbele katika Michezo

Image
Na. Nancy Kivuyo, IPALA Hamasa ya serikali katika michezo nchini ni kichocheo cha wananchi wa Kata ya Ipala kupenda kushiriki michezo ya aina mbalimbali kwa ajili ya kujenga na kuboresha afya zao ili waweze kushiriki katika shughuli za maendeleo. Diwani wa Kata ya Ipala, George Magawa Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Kata ya Ipala, George Magawa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu nafasi ya michezo katika Kata ya Ipala walipotembelea kata hiyo. Diwani Magawa alisema kuwa serikali imekuwa inafanya hamasa kubwa katika michezo hali iliyopelekea kata yao kuwa na mwamko mkubwa katika kushiriki mashindano mbalimbali yanayoandaliwa katani hapo. ā€œKwakweli, mambo ya michezo tunaenda nayo vizuri, kila mwaka tunafanya mashindano yanayoitwa ā€˜Magawa Cupā€™ ambayo diwani ndiye mimi na kwa kushirikiana na mheshimiwa mbunge tuna ā€˜Mavunde Cupā€™, tunaandaa mashindano hayo ili kuwasogeza wananchi karibu zaidi na michezo. Wakati mwingine tunaunganisha michezo na kampeni za kijamii za serika...

Umeme wa REA chachu ya viwanda vidogo vidogo Kata ya Ipala

Image
Na. John Masanja, IPALA Awamu ya kwanza ya umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umechochea shughuli za maendeleo na kuinua uchumi wa wananchi katika Kata ya Ipala, Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Kata ya Ipala, George Magawa wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ā€˜media tourā€™ kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali katika kata hiyo kuanzia mwaka 2021 hadi 2025. Alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imepeleka huduma ya umeme katika Kata ya Ipala. ā€œKata yetu imefikiwa na awamu ya kwanza ambayo ina faida nyingi sana. Wananchi wanafanya shughuli mbalimbali zinazojumuisha matumizi ya umeme kwa kiwango kikubwa na naamini kwa siku za usoni hapa kwetu kutakuwa mtaa wa viwanda vya aina tofautiā€ alisema Magawa. Nae mkazi wa Kata ya Ipala, Mathias Masita aliishukuru serikali kwa kuwapelekea umeme kwasababu maisha yao yamebadilika na wanafanya shughuli zinazohusisha umeme kwa kiwango kikubwa. ā€œMradi wa REA umetunufaisha s...