Kata ya Mkonze yabainisha watoto wenye mahitaji maalum kupata elimu
Na. Coletha Charles, MKONZE Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeendelea na zoezi la kubainisha watoto wenye mahitaji maalum kwa lengo la kujiunga na elimu ya awali na msingi kwa mwaka 2025, kwa ushirikiano na viongozi wa kata, mitaa na wazazi. Akizungumza kuhusu zoezi hilo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Mkonze, Herieth Reuben, alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum kupata fursa za kielimu na kijamii zinazolingana na mahitaji yao. Alisema kuwa kata hiyo ina wakazi 41,000, mitaa nane na shule 12 za msingi. Hivyo, wamejipanga kusimamia shughuli ya uandikishaji kwa asilimia 100 na watapita kila kaya kuwabainisha watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kuanza masomo yao. “Hii ni sehemu ya mpango wetu wa kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata haki zao za msingi bila ubaguzi, tunaomba wazazi watupe ushirikiano ili tuweze kuboresha maswala ya elimu. Lakini pia watoto wengi wenye mahitaji maalum watapata huduma stahiki, watajiunga na elimu ya msingi kwa sababu kata...