Posts

Showing posts from December 5, 2024

Rais, Dkt. Samia aagiza fedha za maadhimisho ya Uhuru kutumika kwenye huduma za kijamii- Majaliwa

Image
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza   Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa Mwaka 2024 yafanyike katika ngazi ya mikoa na Fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya Maadhimisho hayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii. Amesema kuwa kila mkoa uhakikishe Wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira katika maeneo ya kijamii kama vile kwenye Masoko, Hospitali, Kambi za wazee na wenye mahitaji maalum, mashindano ya michezo mbalimbali pamoja na makongamano na midahalo ya kujadili maendeleo endelevu ambayo nchi yetu imefikia katika kipindi cha miaka 63 ya Uhuru.  Amesema hayo leo Jumatano (Desemba 04, 2024) katika kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma. ā€œSherehe za Mwaka huu hazitakuwa na Gwaride na Shughuli nyingine za Kitaifa ā€ . Amesema kuwa Serikali inatoa wito kwa Wananchi kushiriki katika shughuli hiz...