Posts

Showing posts from April 30, 2025

‘Team Aprili’ wapanda miti Shule ya Msingi Mahungu kusherehekea siku yao ya kuzaliwa

Image
Na. Nancy Kivuyo, KIZOTA Watumishi kutoka taasisi mbalimbali za Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamejumuika pamoja kusherehekea mwezi wa kuzaliwa kwa kupanda miti katika Shule ya Msingi Mahungu. Wakitoa hisia zao za furaha walipotembelea shule hiyo mpya, watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma akiwemo Afisa Elimu Kata ya Kiwanja cha Ndege, Mwl. Prisca Mgalula alisema kuwa wameichagua Shule ya Msingi Mahungu ili kuongeza uzuri wa mandhari ya shule hiyo mpya. “Mimi nimezaliwa tarehe 26 Aprili na tumeichagua shule hii kusherehekea kwa kupanda miti takribani 100. Kwa maana hiyo tunaendelea kuhamasisha agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dodoma la ‘Mti wangu, Birthday yangu’ kwa lengo la kuhamasisha wanafunzi kutunza mazingira, lakini pia itawasaidia kujifunzia kwa vitendo hapo baadae" alisema Mwl. Mgalula. Nae, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mahungu, Onesphory Massawe alianza kwa kusema kuwa wanafurahi kuwapokea watumushi hao na wanaahidi kuitunza miti hiyo ili ipendezeshe mandhari ya eneo...

Miti 100 yapandwa S/M Mahungu ‘Mti wangu, Birthday yangu’

Image
Na. Dennis Gondwe, KIZOTA AFISA Elimu Awali na Msingi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Prisca Myalla ameongoza zoezi la upandaji miti 100 katika Shule ya Msingi Mahungu kwa wadau waliozaliwa Mwezi Aprili kwa lengo kuwaandalia mazingira mazuri ya kujisomea wanafunzi shuleni hapo. Alisema kuwa Shule ya Msingi Mahungu ni shule iliyojengwa kwa fedha za serikali kuu kupitia mradi wa Boost awamu ya pili Mwaka wa fedha 2024/2025. Akiongelea zoezi la upandaji miti katika shule hiyo, alisema kuwa ni kuunga mkono juhudi za serikali chini ya kauli hamasishi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ya ‘Mti wangu, Birthday yangu’. “Tupo hapa watumishi tuliojumuika kutoka taasisi mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuanzia walimu, wauguzi hadi maaskari. Sisi ni timu ya watumishi waliozaliwa Mwezi Aprili ‘Team Aprili’. Leo tutapanda miti kutekeleza maono ya mkuu wa mkoa kwamba ‘Mti wangu, Birthday yangu’. Kwa hiyo, tutapanda miti 100 katika eneo hili la shule ili kuendelea kukijanisha Dodoma ye...

Ujenzi Ofisi Kata Mbalawala watakiwa kukamilika kwa wakati

Image
Na. Leah Mabalwe, MBALAWALA Mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Mbalawala watakiwa kukamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma kwa urahisi. Hayo yalizungumzwa na Mhandisi wa Jiji la Dodoma, Mhandisi Ally Bella, katika zoezi la ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyofanywa na Kamati ya Fedha na Utawala robo ya tatu 2024/2025 katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alisema “ninakuagiza Afisa Mtendaji wa kata hii ya Mbalawala kusimamia mradi huu uweze kukamilika kwa haraka kwasababu wananchi wa eneo hili wanategemea ofisi hii kwaajili ya kupata huduma” alisema Mhandisi Bella. Nae, Awadhi Abdallah, Diwani wa Kata ya Zuzu aliishukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kazi nzuri ambayo inaendelea kuifanya katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo. “Binafsi niishukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo, kwasababu kazi za maendeleo zinaendelea kufanyika katika kila maeneno na sehemu ambazo hakuna basi Jiji la Dodo...