Mazoezi ni msingi imara kwa Afya bora
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri amewataka wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuzingatia afya zao kwa kufanya mazoezi na kufuata kanuni bora za kiafya, ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ambayo yameendelea kuongezeka katika jamii. Alitoa wito huo mara baada ya kukamilika kwa Mbio za Kuhamasisha Kupima Afya, mbio hizo zilianzia katika O fisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na kuhitimishwa katika Bustani ya Mapumziko ya Nyerere Square, amba p o kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Upimaji Magonjwa y asiyoambukiza kilifanyika. A lisema kuwa ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha anajilinda dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza. “Nipende kuwasisitiza tu kuwa afya ndio msingi imara na mtaji wa masikini ni nguvu yake mwenyewe . H ivyo , tupambane na tuweke afya zetu vizuri kwa kufanya mazoezi na kupima afya zetu mara kwa mara” alisema Alhaj Shekimweri. Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma , Dkt. Pima Sebastian alisema kuwa...