Mfumo Jumuishi kutoa mikopo ya 10% Jiji la Dodoma
Na. Nancy Kivuyo, TAMBUKARELI Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na Benki ya CRDB wamefanya kikao kazi kuhusu utoaji na usimamizi wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mfumo jumuishi kwa lengo la kujenga uelewa wa Pamoja kuhusu utoaji wa mikopo hiyo. Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Charity Sichona Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Charity Sichona akizungumza na watendaji wa kata na maafisa maendeleo ya jamii, alisema kuwa kanuni na sheria za utoaji wa mikopo kwa vikundi ni muhimu. Aliwataka wazichukue ili wakatoe elimu ya kutosha katika kufanikisha utaratibu wa kupata mikopo kwa haraka na kwa wakati. āMikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu inatekelezwa kwa mujibu wa sheria kwa uwiano wa 4-4-2 ikimaanisha wanawake asilimia nne, vijana asilimia nne na watu wenye ulemavu asilimia mbiliā alisema Sichona. Aidha, aliwasisitiza kuzingatia ...