Jiji lataka mpango kazi kukamilisha ujenzi shule ya Mil. 299,200,000 utekelezwe
Na. Dennis Gondwe, NZUGUNI HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imemuagiza Mkuu wa Shule ya Sekondari Nzuguni kusimamia mpango kazi wa ujenzi wa shule mpya ya msingi ya mkondo mmoja yenye gharama ya shilingi 299,200,000 fedha kutoka mradi wa BOOST ili ikamilike kwa wakati kwa mujibu wa mkataba. Agizo hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alipoongoza timu hiyo kutembelea na kukagua hatua ya ujenzi wa shule hiyo katika Kata ya Nzuguni, jijini Dodoma. Alisema kuwa mpango kazi wa ujenzi wa shule hiyo unatakiwa kufahamika na kila anayehusika na kusimamia utekelezaji wake ili ujenzi ukamilika kwa wakati. Idadi ya mafundi anatakiwa kuongezeka ili kuhakikisha mradi unakamilika haraka, aliongeza. Pia, ilishauriwa manunuzi yote ya vifaa pamoja na madawati yatangazwe kwenye mfumo wa NeST mapema ili kusiwe na ucheleweshaji katika utekelezaji wa mradi. Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa shule mpya ya msingi mkondo mmoja kwa Ti...