Posts

Showing posts from July 15, 2026

Jiji la Dodoma kinara utekelezaji afua za Lishe

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepata alama ya kijani katika kadi alama ya viashiria vya utekelezaji wa afua za lishe ikiwa ni hatua nzuri kwa kipindi cha Robo ya Nne kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026. Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Lishe kwa kipindi hicho, Kaimu Afisa Lishe wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Happiness Mlamka alisema kuwa utekelezaji umeendelea kufanyika kwa mafanikio makubwa ambapo kadi alama ya lishe imeonesha rangi ya kijani. Alisema kuwa rangi hiyo ni kiashiria kwamba halmashauri imefikia viwango vinavyotakiwa katika utekelezaji wa afua za lishe. Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wake, Sakina Mbugi, aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Dodoma alipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuendelea kufanya vizuri katika utekelezaji wa shughuli za lishe. Alisisitiza umuhimu wa kuendeleza utoaji wa elimu ya lishe kwa kutumia kaulimbiu mbalimbali zinazotolewa kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru, ikiwemo “Zingatia lishe yak...

Wadau wa Lishe watakiwa kuzingatia Sheria

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Maafisa lishe na watendaji wa kata wametakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utekelezaji wa shughuli za lishe pamoja na kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa afua za lishe. Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa Robo ya Nne ya Mwaka wa Fedha 2025/2026, Sakina Mbugi alipoongoza kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri. “Katika utekelezaji wa shughuli za lishe ni muhimu kuwashirikisha wadau mbalimbali, wakiwemo viongozi wa dini, wazee na vijana, ili kuwapatia uelewa kuhusu umuhimu wa lishe bora. Tunapompa mzee elimu sahihi ya lishe, tunamsaidia kupunguza changamoto za uzeeni na kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza. Hivyo, nitumie nafasi hii kuwaelekeza maafisa lishe na maafisa watendaji wa kata kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utekelezaji majukumu yenu,” alisema Mbugi. Mw...

Jiji la Dodoma latakiwa kushirikisha wadau afua za Lishe

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetakiwa kuongeza ushirikishaji w a makundi mbalimbali ya jamii katika kuimarisha afua za lishe ili kuhakikisha elimu na huduma za lishe bora zinawafikia wananchi wote. Wito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe kwa Robo ya Nne Aprili-Juni, 2026 Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Sakina Mbugi alipoongoza kikao hicho kwa niaba ya mkuu wa wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri. Mbugi ambae ni katibu tawala wilaya ya Dodoma alisema kuwa ni muhimu kuwashirikisha vijana waliopo nje ya mfumo rasmi, wazee, viongozi wa dini, viongozi wa mila, taasisi za serikali na binafsi, watu mashuhuri pamoja na kaya katika kuhamasisha na kutoa elimu ya lishe bora. Ali sema kuwa ushirikishwaji wa makundi mbalimbali ya jamii ni muhimu katika kuongeza uelewa na kuleta matokeo chanya na kubainisha kuwa lishe bora haih usu watoto pekee bali watu wa rika zote. “Sisi, timu ya wataalam, tupo tayar...

RC Senyamule apongeza ujenzi S/M Goba

Na. Mwandishi wetu, MKONZE SHULE ya Msingi Goba iliyogharimu shilingi milioni 302 imeongeza fursa ya upatikanaji wa elimu bora kwa watoto na kuwapunguzia kutembea umbali mrefu kufuata shule katika maeneo mengine. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Goba iliyopo Mtaa wa Muungano A, Kata ya Mkonze jijini Dodoma. Mkuu wa mkoa aliipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kukamilisha mradi huo unaolenga kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu bora kwa watoto. Vilevile, aliipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa utekelezaji mzuri wa mradi huo na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya elimu ili kukidhi mahitaji yanayotokana na ongezeko la idadi ya watu. “ Nawapongeza kwa kukamilisha ujenzi wa shule hii kwa wakati na kwa viwango vinavyohitajika. Hata hivyo, kutokana na kasi ya ukuaji wa Jiji la Dodoma, ni muhimu kuendelea kujenga miundombinu zaidi ya elimu ili kuhakik...

RC Senyamule aridhishwa maendeleo ya ujenzi Jengo Jumuishi Kituo cha Afya Makole

Na. Mwandishi wetu, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepongezwa kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa mradi wa jengo jumuishi la Kituo cha Afya Makole ukitajwa baada ya kukamilika kuwa utaboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi. Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo jana. Mkuu wa mkoa alisema kuwa kukamilika mradi huo kutaleta mapinduzi makubwa katika utoaji wa huduma za afya katika halmashauri. Alisema kuwa jengo hilo linajengwa eneo la kimkakati katikati ya jiji likizungukwa na taasisi za serikali na binafsi. “Jengo hili litapanua huduma ambazo hazikuwepo hapo awali, ikiwemo huduma za dharura, huduma za uzazi na huduma nyingine za kibingwa. Huu ni mradi muhimu ambao utawawanufaisha wananchi wengi. Niwapongeze sana Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa usimamizi mzuri,” alisema Senyamule. Alitumia wakati huo kuwapongeza watumishi wa Kituo cha Afya Makole kwa kuendelea...

Sekondari Zuzu yapongezwa usimamizi na utunzaji Mazingira

Na. Mwandishi wetu, ZUZU SHULE ya Sekondari Zuzu imepongezwa kwa usimamizi mzuri wa shule na utunzaji wa mazingira jambo linalochochea utulivu wakati wa kufundisha na kujisomea kwa wanafunzi. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipotembelea na kukagua ujenzi wa mabweni mawili katika Shule ya Sekondari Zuzu. Mkuu wa mkoa alimpongeza Mkuu wa Shule ya Sekondari Zuzu, kwa usimamizi mzuri wa shule hiyo. Alisema kuwa shule ina mazingira safi na rafiki kwa wanafunzi kujifunzia kwa utulivu na walimu kuweza kufundisha vizuri jambo lililopelekea shule hiyo kushika nafasi ya tisa kimkoa miongoni mwa shule za serikali. Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Zuzu, Mwl. Hezron Lupondo aliishukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu kupitia uboreshaji wa miundombinu ya shule. “Ujenzi wa mabweni haya mawili umetupa hamasa kubwa sisi walimu na wanafunzi. Mazingira bora ya kujifunzia yanachangia kuongeza ari ya kufundi...