DC Shekimweri awaasa viongozi kutokuchukulia mzaha suala la madada poa
Na. Shahanazi Subeti, DODOMA Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaji Jabir Shekimweri, alitoa maoni kwa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma kufanya utafiti, kutoa elimu na kuweza kujua sababu zinazowafanya wanawake na vijana kufanya biashara ya ngono. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaji Jabir Shekimweri Aliyasema hayo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa kazi robo ya pili kwa kipindi cha Mwezi Oktoba hadi Desemba, 2025 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alhaji Jabir Shekimweri alisema āHalmashauri ya Jiji la Dodoma ina mifuko mahsusi ya vijana na wanawake, hivyo uchunguzi ufanyike kujua kwanini matendo ya uzinifu yanaendelea. Katika kutafuta suluhisho pengine Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani, ingawa taarifa ilipitishwa sioni kama vita ya biashara hiyo ya watu kujiuza katika shughuli za ngono haihitaji ācohesive forceā nguvu ya dola, nadhani inahitaji elimu zaidi na mikakati ya k...