Afisa Biashara Arusha apongeza ukuwaji wa Biashara wa Jiji la Dodoma
Na. Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepongezwa kwa kasi ya ukuaji wa shughuli za biashara na uwekezaji na kutajwa kuwa ni fursa kwa watanzania na wageni kuwekeza. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji Halmashauri ya Jiji la Arusha, John Kilunge alipotembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Kilunge alipongeza kasi ya ukuaji wa shughuli za biashara na uwekezaji ndani ya jiji hilo na kusema kuwa ni fursa kwa watanzania na wageni kuwekeza na kufungua zaidi fursa za ajira. Akiwa katika banda hilo, alipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo, hususan katika sekta za ardhi, biashara na maendeleo ya kiuchumi. Alisema kuwa Jiji la Dodoma linaonesha mafanikio makubwa katika kukuza mazingira ya biashara na kuvutia wawekezaji k...