KAMATI YA SIASA KATA YA MSALATO YATAKIWA KUSIMAMIA MIRADI
Na. Dennis Gondwe, MSALATO KAMATI ya Siasa ya Kata ya Msalato imetakiwa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata ili kujiridhisha ya thamani ya fedha. Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma, Charles Mamba alipoongoza Kamati ya Siasa Wilaya ya Dodoma kutembelea na kukagua ujenzi wa mabweni mawili, vyumba saba vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato iliyopo Kata ya Msalato jijini hapa. Mamba alisema kuwa Kamati ya Siasa Kata ya Msalato ina wajibu wa kufuatilia na kusimamia miradi yote ya maendeleo inayotekelzwa katika kata hiyo. “Kamati ya Siasa Kata ya Msalato mradi huu ni wa kwenu, msisubiri Kamati ya Siasa Wilaya ya Dodoma kuja kukagua. Lazima muwe mnapanga ratiba zenu kukagua miradi hii. Serikali ya awamu ya sita inaleta fedha nyingi kwenye kata kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo, jukumu lenu ni kusimamia utekelezaji wake na thamani ya fedha ionekan...