Posts

Showing posts from June 23, 2026

Katibu Mkuu Uchukuzi aipa tano TASAC kwa kuendelea kuwafikia wadau

Image
Na. Immaculate Ruzika, DODOMA Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, leo ametembelea banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.   Akiwa katika banda hilo, Prof. Kahyarara alipatiwa maelezo kuhusu juhudi za TASAC katika kuhakikisha usalama, ulinzi na ubora wa huduma za usafiri wa majini kwa wananchi. Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, Prof. Kahyarara aliipongeza TASAC kwa kushiriki maonesho hayo na kutumia jukwaa hilo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu na huduma zake kwani elimu hiyo inasaidia kuongeza uelewa na kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi na wananchi. Maonesho hayo yenye kauli mbiu ya "Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu" yalianza rasmi tarehe 16 na yanataria kufika tamati kesho tarehe 23 juni, 2026.

Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali Inafanya Kazi Kubwa – Prof. Kahyarara

Image
Aipongeza Wizara ya Habari Maandalizi AFCON 2027 Na. Adelina Johnbosco - MAELEZO Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, ameipongeza Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali na kusema inafanya kazi kubwa ya kuzitangaza shughuli zinazotekelezwa na Serikali pamoja na kuwafikia wananchi.   Prof. Kahyarara alisema hayo Juni 22, 2026, alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na taasisi zake katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kwenye viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma. "Serikali ina shughuli nyingi zinazofanyika ikiwemo miradi mbalimbali, mipango na malengo kwa ajili ya maendeleo na maslahi ya wananchi, hata ukisema kila siku au kila wiki utoke na kitu kimoja lakini bado inakuwa haitoshi, lakini Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali inajitahidi kwa kufanya kazi kubwa kwani taarifa zinatolewa kuhusu yanayotekelezwa na Serikali kwa wananchi wake" aliongeza Prof. Kahyarara. Kwa upande mwingine, aliipongeza...

Zaidi ya wananchi 300 watembelea banda la TARURA Wiki ya Utumishi wa Umma

Image
# Wananchi wa Kimara kunufaika na ujenzi wa barabara ya TRA - King'ongo   Na. Mwandishi wetu, DODOMA ZAIDI ya wananchi 300 wametembelea banda la Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) tangu kuanza kwa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, wakipata elimu na ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara za wilaya katika maeneo yao. Hatua hiyo imeendelea kuimarisha uhusiano kati ya wananchi na taasisi hiyo, huku ikitoa fursa ya kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi moja kwa moja. Akizungumza katika maonesho hayo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Catherine Sungura alisema kuwa wananchi wanaowasilisha kero zao huunganishwa moja kwa moja na mameneja wa maeneo husika ili kupata maelezo ya kina na ufumbuzi wa haraka. “Tunawapokea wananchi wengi kutoka maeneo tofauti ya Tanzania ambao wengi wanataka kufahamu ujenzi au matengenezo ya barabara katika maeneo yao na hivyo wengi wao wanapata majibu hapo hapo kwani wan...