Posts

Showing posts from April 21, 2024

Mikopo ya Makundi Maalum kurejeshwa Julai, 2024

Image
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kurejesha utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu utakaoanza Julai, 2024. Akiwasilisha bungeni utekelezaji wa bajeti ya Mwaka 2023/24 na makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2024/25, Mchengerwa mikopo hiyo itaanza kwa utaratibu wa kutumia benki kwa halmashauri 10 za majaribio ambazo ni Dar  es Salaam, Dodoma, Kigoma Ujiji na Songea, Miji ya Newala na Mbulu, Wilaya za Siha, Nkasi, Itilima na Bumbuli. Aidha, alisema halmashauri 174 zilizobaki zitatumia utaratibu ulioboreshwa ili kuondoa mapungufu yaliyosababisha changamoto za awali kwa kufanya mambo yafuatayo; uanzishwaji wa kitengo cha usimamizi wa mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika Ofisi ya Rais – TAMISEMI, na uanzishwaji wa kamati za usimamizi wa mikopo katika ngazi za ofisi za wakuu wa mikoa, halmashauri na kata. “M...