Posts

Showing posts from April 16, 2025

Jiji la Dodoma kutekeleza mradi wa urejeshaji taka

Image
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya JUZA, Nasibu Kitabu kwa kushirikiana na Kampuni ya Global Waste Solutions watambulisha mradi wa uchakataji na urejeshaji wa taka kwa Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kupunguza kiwango cha taka zinazopelekwa katika Dampo la Chidaya. Aliyazungumza hayo katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri na kusema kuwa taasisi hiyo imejikita katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira pamoja na kutoa elimu kwa vijana wanaofanya kazi ya kuzoa taka. “Kwasasa tupo katika Jiji la Dodoma na tumeungana na Global Waste Solutions kufanya hii kazi ili kupunguza kiasi kikubwa cha taka kwenda dampo ifikapo mwaka 2027. Yote hii ni kuweza kuifundisha jamii namna ya kutenganisha taka ili tuweze kuiokoa jamii yetu na changamoto zitokanazo na utunzaji na utupaji holela wa taka” alisema Kitabu. Aliongeza kuwa Jiji la Dodoma limekuwa kwa kasi na ndipo ilipo sura ya nchi. “Jili la Dodoma ni fahari ya watanzania, tumeona ni vem...

Wananchi Kata ya Kikuyu Kaskazini wafurahia huduma ya kujifungua Zahanati ya Kikuyu

Image
Na. Leah Mabalwe, KIKUYU KASKAZINI Kata ya Kikuyu Kaskazini yajivunia maboresho ya huduma za afya kwa kina mama jambo linalopunguza uwezekano wa vifo vya kina mama wajawazito na wakati wa kujifungua katika Zahanati ya Kikuyu. Akiongea na waandishi wa habari waliotembelea Zahanati ya Kikuyu kujionea utoaji wa huduma katika jengo la wazazi ikiwa ni ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali kwa kipindi cha miaka minne kwenye Kata ya Kikuyu Kaskazini. Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kikuyu, Dkt. Azania Silliah alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, kwa kuwapatia shilingi 33,612,800 kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa jengo la wazazi. Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma aliwapatia shilingi 50,000,000 kwaajili ya umaliziaji wa jengo hilo. “Napenda kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kwa kuona umuhimu wa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi. Nipende kumshukuru Mbunge wetu, Anthony Mavunde kwa kuwa mstari wa mbele kwaajili ya kuhaki...