MADIWANI JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTATUA KERO ZA WANANCHI
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma watakiwa kusikiliza kero za wananchi na kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati ili kuimarisha maendeleo na ustawi wa jamii. Hayo aliyasema Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaji Jabir Shekimweri, wakati alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Alisema kuwa madiwani ni kiungo muhimu kati ya serikali na wananchi, hivyo wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao. “Madiwani ni sauti ya wananchi. Ni muhimu msikilize kwa umakini kero zao na kuzitatua kwa wakati ili kuondoa malalamiko yasiyo ya lazima na kuongeza imani ya wananchi kwa serikali yao” alisema Alhaji Shekimweri. Aliongeza kuwa utekelezaji wa majukumu hayo unahitaji uwajibikaji, ushirikiano na ufuatiliaji wa karibu wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha inaleta matokeo yaliyokusudiwa. Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya ...