Posts

Showing posts from May 16, 2026

Hazina Volleyball yaiduwaza Dodoma Jiji Seti 2-0 Mwenge Super Cup

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA TIMU ya Wanaume ya Mpira wa Mikono ya Hazina (Hazina Volleyball Club) imeibuka na ushindi wa Seti 2-0 dhidi ya Timu ya Dodoma Jiji mchezo uliochezwa katika viwanja vya Chinangali Park mapema leo. Akiongelea mchezo huo, Nahodha wa Timu ya Hazina Volleyball Club, George Kalunde alisema timu yake ilijiandaa vizuri kuelekea mchezo huo ndio sababu ya kupata ushindi wa Seti 2-0. Aidha, aliipongeza Wilaya ya Dodoma kwa kuandaa mashindano ya Mwenge Super Cup Mwaka 2026 na kutaja maandalizi hayo kuwa ni ubunifu mkubwa. “Nitumie nafasi hii kuwahamasisha vijana wenzangu kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mapokezi na mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 katika Wilaya ya Dodoma, karibuni sana. Nae Nahodha wa Timu ya Mpira wa Mikono ya Dodoma Jiji, Muhidin Mwenda alisema kuwa mchezo ulikuwa mzuri pamoja na kufugwa. “Tunapenda kumshukuru Mungu tumemaliza mechi salama, pamoja na kuwa tumepoteza mechi kwa seti 2-0, siyo matokeo mazuri kwetu. Mashindano haya yamekuwa c...

Dodoma Jiji yaangukia pua dhidi ya Ujenzi Queens Mwenge Super Cup

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA TIMU ya Mpira wa Pete ya Wizara ya Ujenzi (Ujenzi Queens) imeibuka kidedea kwa kuifunga Timu ya Mpira wa Pete ya Dodoma Jiji kwa magoli 37-33 katika mchezo wa kuvutia uliochezwa katika viwanja vya Chinangali Park. Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kawaida na kuendelea kushika kasi kadri muda ulivyokuwa ukisogea. Hadi mchezo unamalizika, Timu ya Ujenzi Queens iliikuba na ushindi wa magoli 37 dhidi ya 33 ya Dodoma Jiji. Awali Kocha wa Timu ya Mpira wa Pete ya Ujenzi Queens Mwamvita Mzee alisema kuwa wamekuwa wakipata matokeo mazuri kutokana na kufanya mazoezi mara kwa mara. “Timu yetu inaamini katika mazoezi ya mara kwa mara. Kama unavyofahamu mazoezi hayadanganyi, tumekuwa tukifanya mazoezi kwa bidii ndiyo siri ya mafanikio yetu. Zidi ni kupendana kama timu na watu kujitoa kwa ajili ya timu na kuupenda mchezo. Pia, kwetu ni utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Tanzania ya kufanya mazoezi kwa watumishi mahala pa kazi” alisema Mzee.   Kwa upa...

Ujenzi Queens bega kwa bega na Mwenge wa Uhuru, 2026 Dodoma

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA WIZARA ya Ujenzi inaunga mkono Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 utakaoanza mbio zake tarehe 1 Juni, 2026 katika Wilaya ya Dodoma kwa kushiriki katika mashindano ya Mwenge Super Cup yakilenga kuhamasisha jamii kujiandaa na mapokezi ya Mwenge huo kwa kudumisha amani na umoja wa kitaifa. Kocha wa Timu ya Wizara ya Ujenzi (Ujenzi Queens), Mwamvita Mzee Kauli hiyo ilitolewa na Kocha wa Mchezo wa Mpira wa Pete wa Timu ya Wizara ya Ujenzi (Ujenzi Queens), Mwamvita Mzee alipokuwa akiongea na mwandishi wetu muda mfupi kabla ya kuanza mchezo wao na Timu ya Mpira wa Pete ya Dodoma Jiji katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma. Mzee alisema kuwa hamasa ya Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 kwa wanamichezo ni kubwa katika Wilaya ya Dodoma. “Sisi Timu ya Mpira wa Pete ya Wizara ya Ujenzi tumehamasika kuja kuunga mkono ujio wa Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 katika Wilaya ya Dodoma. Lengo ni kuonesha umoja na mshikamano baina ya wanamichezo kama dhamira ya Mwenge wa Uhuru Mwaka 2...