TANZANIA NA KOREA KUSINI KUSHIRIKIANA UTAFITI WA KILIMO NA TEKNOLOJIA YA KISASA YA KILIMO
.jpeg)
Nchi za Tanzania na Korea Kusini zimekubaliana kushirikiana katika kuimarisha utafiti wa kilimo na matumizi ya teknolojia ya kisasa ya kilimo ili kuongeza tija kwa wakulima wa Tanzania. Hayo yamesemwa leo Mjini Jeonju-si, Korea Kusini wakati wa mazungumzo ya ushirikiano baina ya Naibu Waziri wa Kilimo wa Tanzania, Mh. Anthony Mavunde na Ndg. Yun Jongchul Makamu Mtawala Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Kilimo na Utafiti ya Korea (Korea Patnership for Innovation in Agriculture- KOPIA). Kupitia mazungumzo hayo Naibu Waziri Mavunde ameiomba KOPIA kuanzisha kituo chake nchini Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) ili kubadilishana uzoefu na kuongeza ufanisi katika tafiti za kilimo kwa lengo la kumsaidia mkulima kulima kwa tija na kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa kutumia kanuni bora za kilimo,uzalishaji mbegu bora na teknolojia ya kisasa ya kilimo,sambamba na hayo Naibu Waziri Mavunde ameomba pia ushirikiano wa kitaalamu katika utekelezaji wa P...