Posts

Showing posts from June, 2026

Wilaya ya Dodoma yapata “clean sheet” Miradi ya Mwenge wa Uhuru 2026

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA Jumla ya miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bil. 9,823,862,925 iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 katika Wilaya ya Dodoma imepitishwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 ili iweze kutoa huduma kwa wananchi. Miradi iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 ni mradi wa Nishati safi ya kupikia katika Shule ya Sekondari Dr. Samia-Dodoma wenye thamani ya shilingi 698,800,161, mradi wa uwekezaji binafsi wa Hoteli ya Starline wenye thamani ya shilingi 3,000,000,000 ukiwa pamoja na kutembelea mradi wa kusimika kamera za usalama wenye gharama ya shilingi 682,561,548, mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa Shule ya Sekondari Wella wenye thamani ya shilingi 42,800,000, mradi wa Maji safi Kata ya Nala unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira na ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilimeta 1.6 kutoka Barabara iendayo Singida hadi Hospitali ya Jiji wenye thamani ya shilingi 2,872,857,6...
Na. Dennis Gondwe, TAMBUKARELI HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetumia shilingi 519,891,609 kwa ajili ya kusimika mfumo wa kamera za usalama ili kuwahakikishia ulinzi na usalama wananchi na mali zao pamoja na wawekezaji. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya mradi wa kusimika kamera za usalama jijini Dodoma kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2026 tukio lililofanyika katika Hoteli ya Starline jijini Dodoma. Akiongelea lengo la mradi huo, alisema kuwa ni kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao. “Kamera hizi zinalenga kulinda miundombinu ya Umma katika Jiji la Dodoma, kudhibiti makosa ya barabarani na matendo ya uhalifu. Aidha, mradi utasaidia kutoa uhakika wa usalama kwa wadau wa shughuli za maendeleo na kulifanya Jiji la Dodoma kuwa salama kwa shughuli za uwekezaji, kidiplomasia, utalii na kuhakikisha Jiji linaendeshwa kidijitali” ...

Shilingi 698,800,161 zatekeleza mradi wa Nishati safi Sec Dr. Samia- Dodoma

Na. Dennis Gondwe, IYUMBU SHILINGI 698,800,161 za utekelezaji wa mradi wa Nishati safi ya kupikia katika Shule ya Sekondari Dr. Samia-Dodoma zimelenga kuhifadhi Mazingira kwa kurejesha taka, kupunguza matumizi ya kuni na mkaa na kulinda afya za watumiaji. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Dr. Samia-Dodoma, Mwl. Leticia Singo alipokuwa akisoma taarifa ya mradi wa nishati safi ya kupikia kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2026 shuleni hapo. “Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, l engo la mradi ni kuhifadhi Mazingira kwa kurejesha taka zinazozalishwa shuleni pamoja na kupunguza madhara yatokanayo na matumizi ya kuni na mkaa kwa kutumia nishati safi ya kupikia” alisema Mwl. Singo. Alisema kuwa mradi huo ulitekelezwa kwa gharama ya shilingi 698,800,161 fedha kutoka mradi wa P4R chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia chini ya Mkandarasi SUMA JKT. Akiongelea mafanikio ya mradi huo, aliyataja kuwa ni mradi umepunguza gharama z...

Jiji la Dodoma latenga Bil. 3.9 kuongeza miundombinu mapokezi ya Kidato cha Kwanza 2027

Image
Na. Dennis Gondwe, KIKUYU KUSINI HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetenga shilingi 3,956,990,000 katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2026/2027 kwa ajili ya kuongeza miundimbinu ya madarasa, viti, meza na matundu ya vyoo ikiwa ni maandalizi ya kupokea wanafunzi watakaohitimu darasa la sita na saba kwa pamoja. Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Wella, Mwl. Allen Lugemalila wakati a kisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Wella kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2026, shuleni hapo. “ Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, h almashauri inategemea kupokea wanafunzi watakaohitimu darasa la sita na la saba kwa pamoja mwaka 2027. Katika kufanikisha mpango huo wa serikali, kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027, halmashauri imetenga bajeti ya shilingi 3,956,990,000 kwa lengo la kuongeza miundombinu ya madarasa, vyoo, viti na meza. Pamoja na lengo hili la msingi, shule hii ilikuwa na uhitaji wa vyum...

Mamia wajitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru 2026 Kata ya Kikuyu Kusini

Image
Na. Dennis Gondwe, KIKUYU KUSINI MAMIA ya wananchi wa Kata ya Kikuyu Kusini wamejitokeza wa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru ulipowasili katika Shule ya Sekondari Wella kuzindua mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa wenye thamani ya shilingi 42,800,000 fedha kutoka mapato ya ndani ya halmashauri. Akiongelea wingi huo wa wananchi, Afisa Mtendaji Kata ya Kikuyu Kusini, Violet Oswald alisema kuwa muitikio wa wananchi kujitokeza kwa wingi utekelezaji wa misingi ya Mwenge wa Uhuru ya kuwaleta watu pamoja kwa upendo na kusisitiza umoja na mshikamano. “Wingi huu wa wananchi wa Kata ya Kikuyu Kusini ni utekelezaji wa kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 isemayo ‘Tanzania ni yetu sote, tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo’. Hivyo, wananchi wamejitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wao na kushuhudia unavyozindua madarasa yao yaliyojengwa kwa fedha zao” alisema Oswald. Akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Wella kwa Kiongozi wa M...

Mwenge wa Uhuru 2026 wakabidhi gari la shilingi 121 Kikundi cha Vijana

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2026, Wazo Mwang’onda ametembelea na kukabidhi gari lenye thamani ya shilingi 121,871,152.50 fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kupitia mkopo ya asilimia nne kwa kundi la vijana baada ya kujiridhisha na utendaji kazi wa Kikundi cha Mwamko wa Vijana Kiuchumi. Tukio hilo lilifanyika katika Shule ya Sekondari Umonga baada ya kupokea taarifa ya Kikundi cha Mwamko wa Vijana Kiuchumi (MVK) na kushuhudia makala fupi ya safari na shughuli za kikundi. Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa Wazo Mwang’onda alisema kuwa utaratibu wa serikali kutoa mikopo isiyo na riba kwa vijana ni uamuzi bora. Lengo la mikopo hii ni kuwakomboa vijana kwa kuwapatia mitaji kwa ajili ya kuendesha biashara na kufanya shughuli za kujiongezea kipato. Aidha, aliwapongeza vijana hao kwa ubunifu wao katika kutekeleza majukumu yao. Akisoma taarifa ya mradi wa Kikundi cha Mwamko wa Vijana Kiuchumi kinachojishughulisha ...