Sekta binafsi kugharamia miradi Jiji la Dodoma Bajeti ya 2025/2026
Na. Faraja Mbise, DODOMA Sekta binafsi itashiriki kugharamia miradi ya maendeleo kwa njia ya ubia katika utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 kutokana na umuhimu wa sekta hiyo kwa maendeleo ya Jiji la Dodoma. Katibu wa Baraza la Madiwani, Dkt. Frederick Sagamiko Mapendekezo ya Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma, imeshirikisha sekta binafsi kutokana na matamanio na mahitaji kuwa makubwa kuliko makusanyo ya mapato. Hayo yalisemwa na Katibu wa Baraza la Madiwani ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko, alipokuwa anatolea ufafanuzi katika baadhi ya masuala yaliyowasilishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani maalum kwa ajili ya kupokea na kupitia mapendekezo ya rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma tarehe 30 Januari, 2025. Dkt. Sagamiko alisema “ matamanio yetu na mahitaji yetu ni makubwa kul...