Mbunge Mavunde awakumbuka mama lishe Dodoma
Na. Faraja Mbise, DODOMA Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde, ameahidi kuwatengenezea mazingira mazuri na rafiki ya kufanyia biashara mama lishe waliopo pembezoni mwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Mavunde alizungumza hayo mara baada ya kumaliza zoezi la uzinduzi wa ujenzi wa jengo la kupumzikia wananchi lilipo nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Aidha, Mavunde aliahidi kuwaboreshea na kuwatengenezea mazingira rafiki ya kufanya biashara ya chakula na kukarabati miundombinu kama vile kuwatengenezea meza na viti za kufanyia biashara pamoja na kuweka maeneo nadhifu. Mavunde alisema “sambamba na hilo nafahamu ya kwamba, asilimia kubwa ya wanaokaa pale hawavimudu vyakula ambavyo watu wengi hapa tunavimudu vyakula vya mahotelini...”. Hata hivyo, Mavunde aligusia wananchi wa kipato cha chini wasioweza kumudu gharama kubwa za kununua chakula kwa ajili ya wagonjwa wao hivyo kuahidi kuwasaidia mama lishe kuboresha maeneo yao ya kufanyia kazi kuwa safi na sal...