Vijana wajitokeze kujiandikisha Daftari la kudumu la wapiga kura
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA VIJANA katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kujitokeza kwa wingi leo kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili watumie haki yao ya kikatiba ya kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani katika uchaguzi mkuu ujao. Ushauri huo ulitolewa na Mwandishi wa Habari Mwandamizi kutoka Uhondo TV, Fadhili Komba muda mfupi baada ya kujiandikisha katika kituo cha Zahanati ya Reli kilichopo Kata ya Tambukareli, Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Komba alisema kuwa vijana wanawajibu wa kujitokeza kwa wingi ili kutumia haki yao ya kikatiba na kidemokrasia. “Ikiwa leo ni siku ya mwisho ya uandikishaji kwa ajili ya kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma muda bado upo wa kutosha. Kijana mwenzangu haujachelewa, wahi sasa ukajiandikishe au kuboresha taarifa zako. Tukumbuke vijana ndiyo nguvu kazi ya taifa” alisema Komba. Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma ukihusi...