MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MISA TAKATIFU YA UPADIRISHO JIMBO KATOLIKI DODOMA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. Philip Mpango ameungana na waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa Kanisa
katoliki kushiriki katika Misa Takatifu ya Upadirisho pamoja na Ufunguzi wa
Mwaka wa Jubilei ya Miaka 50 ya Parokia ya Kiwanja cha Ndege mkoani
Dodoma.
Misa hiyo Takatifu imefanyika katika Kanisa Katoliki la
Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege na kuongozwa na Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Askofu Beatus Kinyaiya.
Askofu Kinyaiya aliwasisitiza waumini kujitokeza katika
kupiga kura kuchagua viongozi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu
watakaowatumikia kwa miaka mitano ijayo. Pia ametoa rai ya matumizi sahihi ya
akili mnemba (AI) ili kuepusha maovu na udanganyifu katika jamii.
Jumla ya Mashemasi watatu wamepata daraja la Upadre
katika Misa hiyo ambao ni Padre Joseph Ibrahim, Padre Sajilo Mark pamoja Padre
Damian Mtanduzi.
Aidha, Misa hiyo imeambatana na uwekaji wa Jiwe la Msingi
ujenzi wa jengo la Katekesi (Jengo la kufundishia dini) lililopo katika Parokia
hiyo ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska – Kiwanja cha Ndege.
Chanzo: Blog ya Fullshangwe
Comments
Post a Comment