Mila na Desturi kandamizi mwiba kwa mtoto wa kike
Na. Faraja Mbise, DODOMA Tanzania inaungana na mataifa mengine katika kupambana na changamoto ya mila na desturi kandamizi ambazo ni kikwazo kwa mtoto wa kike katika kutimiza ndoto zake hasa katika suala la uongozi. Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani yaliyofanywa na Shirika la Msichana Initiaves, jijini Dodoma, Balozi. Liberata Mulamula alisema kuwa am tot desturi kandamizi ni kikwazo kwa binti katika kuzifikia ndoto zake hasa katika uongozi. Balozi Mulamula alisema “mila na desturi kandamizi zinamyima mtoto wa kike haki yake ya msingi ya kwenda shule kusoma. Kwahiyo, zinapunguza idadi ya wanawake kuwa viongozi. Mila na desturi kandamizi ndani ya jamii zinampa mtoto wa kike machaguzi machache ambayo yanapelekea kupoteza watoto wa kike wengi sana”. Aidha, alisisitiza mtoto wa kike kutumia teknolojia kwa lengo la kujifunza na kuelimika hasa katika mitandao ya kijamii. Aliwataka waitumie waitumie kwa ufasaha katika kupata elimu na kuwataka kujitambua n...