TAKUKURU yapewa rai kuboresha mikakati ya kutokomeza rushwa
Na. Nancy Kivuyo , DODOMA Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imeeleza kuwa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania imejipanga kutoa elimu na kusisitiza wananchi kuepuka kupokea rushwa kwaajili ya kuchagua viongozi. Hayo yalielezwa na Mratibu wa Banda la TAKUKURU, Suzana Raymond wakati akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma aliyetembelea banda hilo katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea Nzuguni jijini Dodoma. Alisema kuwa banda la TAKUKURU limejikita katika kutoa elimu na kupokea taarifa zinazohusu masuala ya rushwa. “ Pamoja na majukumu yote, wakati mwingine tunapokea ushauri mbalimbali kwasababu sisi tunaweza tusione tunachokifanya lakini walio nje ndio wanaona nini tunakifanya na huwa tunapeleka ngazi za juu na wao wanazifanyia kazi kwa kadri inavyotakikana ” alisema Raymond . Alisema k u wa lengo la kuwepo katika maonesho ya Nanenane ni kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa jamii hasa kuelekea uchaguzi mkuu. “Lakini katika...