WAKAZI WA KATA YA NALA WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUPIGA KURA KABLA YA SAA 10 JIONI

Na. Theresia Nkwanga, NALA MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo amewataka wakazi wa Kata ya Nala kujitokeza na kutumia haki yao ya kidemokrasia kupiga kura kumchagua mwakilishi wao. Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo akimsikiliza mpiga kura katika moja ya kituo cha kupigia kura Kata ya Nala Kayombo alisema hayo katika kituo cha Sengu chini apokuwa akitoa muhtasari wa hali ya uchaguzi mdogo wa Diwani Kata ya Nala unaoendelea katika vituo 12 vya kata hiyo. “ Leo tarehe 19 Septemba, 2023 Kata ya Nala inafanya uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi ya aliyekuwa Diwani aliyefariki. Zoezi la kufungua vituo lilifanyika kama sheria inavyotaka saa 1:00 asubuhi. Mpaka sasa saa 6 mchana zoezi la upigaji wa kura linaendelea vizuri na wananchi wamejitokeza kwa wingi kuja kuchagua mwakilishi wao. Niwaombe wananchi waendelee kujitokeza muda bado sasa ni saa 6 mchana hadi saa 10 jioni ndio tunafunga vituo” alisema Kayombo. Aidha, aliwataka wananchi wa...