Posts

Showing posts from September 5, 2026

Vijana Dodoma na Iringa Kukutana Kupaza Sauti Dhidi ya Rushwa

Image
Na. Muhamad Said, IRINGA Wanafunzi kutoka klabu za wapinga rushwa za shule za msingi na sekondari za mikoa ya Dodoma na Iringa leo wanatarajiwa kukutana katika mdahalo maalumu wa mapambano dhidi ya rushwa. Mdahalo huo utafanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Lugalo, mkoani Iringa, ukilenga kuwajengea wanafunzi uelewa, kuimarisha maadili na kuongeza ushiriki wa vijana katika mapambano dhidi ya rushwa ndani ya shule na jamii kwa ujumla. Kupitia mdahalo huo, wanafunzi wanatarajiwa kutoa hoja kuhusu madhara ya rushwa kwa jamii na taifa pamoja na changamoto zinazoweza kujitokeza katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo. Aidha, mjadala unatarajiwa kutoa nafasi kwa vijana kueleza namna wanavyoweza kuwa sehemu ya mabadiliko katika kujenga jamii inayozingatia uadilifu. Ushirikishwaji wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari unatarajiwa pia kuifanya shughuli hiyo kuwa sehemu ya kuwaandaa vijana kuwa mabalozi wa maadili na mapambano dhidi ya rushwa, kwa kuanza kujenga uelewa na msi...

RC Kheri James: Elimu iwe silaha yenu dhidi ya rushwa

Image
Na. Muhamad  Said, IRINGA Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James amewataka wanafunzi wa klabu za wapinga rushwa kutoka mikoa ya Iringa na Dodoma kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa, akisisitiza kuwa elimu na uadilifu ni msingi muhimu wa kujenga taifa lenye maendeleo endelevu. Akizungumza katika mdahalo wa klabu za wapinga rushwa za shule za msingi na sekondari unaofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Lugalo, amewahimiza wanafunzi kutambua madhara ya rushwa na kuanza mapema kujenga utamaduni wa kuikataa, akieleza kuwa kizazi cha leo ndicho kitakachobeba dhamana ya uongozi na maendeleo ya taifa hapo baadaye.   Alisisitiza kuwa suala la kupinga rushwa linapaswa kupigwa vita na watu wote wakiwemo wanafunzi, akiongeza kuwa vijana wanapaswa kuwa mabalozi wa uadilifu katika shule zao, familia na jamii kwa ujumla kwa kukataa vitendo vya rushwa na kuhamasisha wenzao kusimamia haki na uwajibikaji.   Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wanafunzi kutumi...

LAAC yalipongeza Jiji la Dodoma kwa ubunifu wa Jengo Jumuishi Kituo cha Afya Makole

Image
Na. Mwandishi Wetu, VIWANDANI   Halmshauri ya Jiji la Dodoma imepongezwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kwa ubunifu wa kujenga jengo jumuishi la huduma za afya la ghorofa tatu katika Kituo cha Afya Makole lenye gharama ya shilingi bilioni 6.9 hatua inayolenga kutatua changamoto ya uhaba wa eneo na kukidhi ongezeko la mahitaji ya huduma za afya katika jiji hilo.   Pongezi hizo zilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa (LAAC), Abdallah Chikota wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kukagua miradi ya maendeleo Kata ya Viwandani Jiji la Dodoma.   Chikota alisema kuwa mfumo wa kujenga ghorofa ulikuwa ndio mbadala sahihi wa kukabiliana na changamoto ya uhaba wa eneo na kupanua huduma za matibabu, bila kulazimika kutafuta eneo jipya nje ya kituo hicho cha afya.   “Kwanza tunalipongeza Jiji la Dodoma kwa ubunifu wao na mawazo ya kisasa kwa sababu hapa Kituo cha Afya Makole kuna changamoto ya eneo, kwa hiyo ili kutatua tatizo hilo wameamu...

LAAC yaridhishwa, yalipongeza Jiji la Dodoma ujenzi wa Barabara ya KM 1.6

Image
Na. Maandishi wetu, NALA   Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imelipongeza Jiji la Dodoma kwa ukamilishaji wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 1.6 inayoelekea Hospitali ya Jiji na kuufanya mradi huo kuwa wa kipekee ukilinganishwa na miradi iliyotekelezwa katika maeneo mengine.   Akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kukagua miradi ya maendeleo Makamu Mwenyekiti wa LAAC, Abdallah Chikota, alisema kuwa kamati imeridhishwa na ubora wa utekelezaji wa mradi huo uliogharimu shilingi bilioni 2.8 kwa kutumia mapato ya ndani ya Jiji la Dodoma.   Alisema kuwa uwekaji wa miundombinu ya usalama ikiwamo taa za barabarani ni hatua muhimu inayoongeza thamani ya mradi na kurahisisha wananchi kufika Hospitali ya Jiji wakati wowote. Aidha, uwekaji wa taa, mitaro na alama za barabarani umeboresha mpangilio na matumizi salama ya njia hiyo.   “Mradi umejengwa kwa kiwango ambacho tumeridhika. Pia, tumeridhishwa na hatu...