Twende Butiama kupambana na ujinga, umasikini na maradhi Jiji la Dodoma
Na. Faraja Mbise, DODOMA MAKULU Waendesha baiskeli wamuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Nyerere kwa lengo la kupambana na maadui watatu wa maendeleo ambao ni maradhi, umasikini na ujinga kwa kugawa madawati 100 katika Shule ya Msingi Dodoma Makulu iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Mwenyekiti wa msafara Twende Butiama Gabriel Landa, alisema kuwa msafara huo una lengo la kumuenzi Baba wa Taifa kwa vitendo kwasababu Mwl. Julius Nyerere alitumia chombo cha baiskeli wakati alipokuwa mwalimu na hata alipoacha uwalimu na kuanza harakati za kupigania uhuru na mambo mbalimbali alitumia baiskeli. Mwalimu Nyerere pia aliwahi kusafiri kwa kuendesha baiskeli kutoka Dar-es-Salaam hadi Arusha, aliongeza. Msafara huo umewaunganisha watu wa nchi mbalimbali kwa kuonesha Mwalimu Nyerere alikuwa sio mbinafsi bali mpenda umoja. “Wengi wanaotuona barabarani wanahisi haya ni mashindano ila haya sio mashindano bali ni msafara wa kawaida ambao tunaendesha baiskeli kwa mwendo wa upendo am...