Afisa Biashara Jiji la Dodoma aelezea umuhimu wa kuanzisha Kanda za Huduma
Na. Ramla Makamba, HOMBOLO BWAWANI Katika kuhakikisha huduma za mapato zinapatikana kwa urahisi na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato halmashauri ya Jiji la Dodoma imeanzisha mfumo wa kanda zitakazohudumia wakazi wa kata mbalimbali kwa karibu ambapo wataalamu watakuwa katika maeneo mbalimbali kutoa huduma hizo zikiwemo huduma za ukataji wa leseni ambapo mpango huo utaanza mapema mwezi Agosti, 2025. Wananchi watapata huduma kama vile za ulipaji wa tozo mbalimbali katika maeneo yao bila kulazimika kufuata huduma Katikati ya jiji ikiwa ni miongoni mwa harakati za kutatua changamoto za umbali wa upatikanaji wa huduma pamoja na kuhakikisha ukusanyaji thabiti wa mapato ya serikali ambapo mwanzoni yalikuwa hayafanywi kikamilifu. Hayo yalisemwa na Afisa Biashara wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fikiri Mtoi, katika kikao kilichofanyika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Bwawani jengo la utawala, na kuhudhuriwa na watendaji wa kata, watendaji wa mitaa, wenyeviti wa mitaa na wadau wa b...