RC Dendego apeleka salamu za Waziri Bashe Nanenane
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego aeleza kuwa Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau itaendelea kutekeleza vipaumbele vya kilimo ili kuongeza tija za uzalishaji, kuchangia ongezeko la ajira pamoja na ushiriki wa vijana na wanawake katika sekta ya kilimo. Aliyasema hayo wakati akisoma salamu za Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati wa ufunguzi wa maonesho Nanenane ya wakulima, wafugaji na wavuvi uliofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma kuanzia tarehe 01 – 08 Agosti, 2025. Alisema kuwa zipo hatua zitakazosimamiwa na wizara katika kuhakikisha nchi inakua na chakula cha kutosha wakati wote. “Wizara inatazamia kuimarisha upatikanaji wa chakula na lishe, kuimarisha upatikanaji wa masoko, mitaji na mauzo ya mazao ya kilimo nje ya nchi. Pia kuimarisha maendeleo ya ushirika na kuimarisha matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika uendelezaji wa sekta ya kilimo” alisema Dendego. Alimalizia kwa kusema kuwa wizara imeendelea kuwashauri, kuwael...