Posts

Showing posts from January 31, 2024

DC Shekimweri awataka wazazi kuwa karibu na watoto wao

Image
Na. Arafa Waziri, DODOMA MAKULU Mkuu wa Wilaya wa Dodoma, Alhaji Jabir Shekimweri aliwataka wazazi kuwa karibu na watoto wao ili kuwaepusha   na vitendo vya kikatili ili wawe katika mazingira salama.   Mkuu wa Wilaya wa Dodoma, Alhaji Jabir Shekimweri akiongea na walimu na wazazi  Aliyasema hayo wakati alipotembelea Shule ya Msingi Kisasa na kuongea na walimu na wazazi shuleni juu ya masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia na uelimu kwa ujumla. Alhaj Shekimweri alisema kuwa ukatili wa kijinsia hutokea katika familia kutokana na kuaminiana sana baina ya wanafamilia. “Upo ukatili wa kijinsia, tafiti zinaonesha ukatili wa kijinsia kwa watoto asilimia kubwa wanafanyiwa na ndugu wa karibu Dunia imebadilika sana hivyo, nawasisitiza hatuna budi kuchukua tahadhari katika kuwaangalia watoto kwa karibu’’ alisema Shekimweri. Alisema kuwa ni vema wazazi kufuatilia mienendo ya watoto wao kwa kuangalia watu wanaokutana na kuhusiana nao ili kubaini kama wanafaa kumjenga mtoto h...

Wazazi watakiwa kutowafisha wanafunzi wenye ulemavu Dodoma

Image
Na. Leah Mabalwe, DODOMA MAKULU   Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaji Jabir Shekimweri amewataka wazazi kutowaficha watoto wenye uhitaji maalum na badala yake kuwapeleka shule kwa sababu nao wanatakiwa kupata elimu iliyo bora.   Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri akikagua kazi za watoto wenye mahitaji maalum Kauli hiyo aliitoa alipokuwa akiongea na Jumuiya ya Shule ya Msingi Dodoma Viziwi alipofanya ziara ya kawaida kutembelea shule hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.   Alhaji Shekimweri alisema kuwa kila mzazi anatakiwa kumpeleka mtoto wake shule hata kama anaulemavu kwasababu ni haki yake ya msingi. “Nitoe kauli hii kwa wazazi wote, kila mtoto asiachwe nyuma, kila mtoto ananafasi ya kupata elimu na sio elimu tu na baadae kuweza kuitumikia nchi katika nafasi mbalimbali. Wazazi wote wasifiche watotot wao wenye changamoto wakakosa nafasi ya kusoma, sio tu mnakuwa hamuwatendei haki watoto bali hamjitendei haki nyie kama wazazi. Wapo waz...