Posts

Showing posts from July, 2026

Timu ya SHIMISEMITA ya Jiji la Dodoma yajipanga kutetea ubingwa

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Kikosi cha Timu ya Watumishi wa Jiji la Dodoma cha Mpira wa Miguu kinaendelea kujifua kwa mazoezi makali kuelekea mashindano ya SHIMISEMITA 2026 yatakayofanyika jijini Mbeya, kikiwa na malengo ya kufanya vizuri na kutwaa ubingwa. Hayo aliyasema Kocha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Watumishi Jiji la Dodoma, Given Aristides wakati wa bonanza la kimichezo lililozikutanisha Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na Halmashauri ya Wilaya ya Gairo katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma, ambapo timu hizo zilipata nafasi ya kupima uwezo wao kabla ya kuingia kambini kwa ajili ya mashindano hayo. Alisema kuwa ushindani katika SHIMISEMITA unazidi kuongezeka kila mwaka kutokana na halmashauri nyingi kujiandaa kwa umakini, jambo linalowalazimu kuongeza kiwango cha mazoezi na nidhamu ili kufikia malengo waliyojiwekea. “Tunafahamu kuwa SHIMISEMITA ni mashindano yenye ushindani mkubwa, hivyo tunaendelea kujinoa kwa bidii kila siku. Bonanza hil...

Timu ya Jiji la Dodoma yajinoa kuelekea SHIMISEMITA Mbeya, 2026

Image
Na. Mwandishi Wetu, Dodoma MSAKO wa kutetea ubingwa wa mashindano ya Shirikisho la Michezo la Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) umeanza rasmi kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma baada ya watumishi wake kushiriki bonanza la michezo lililozikutanisha Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na Halmashauri ya Wilaya ya Gairo katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma. Bonanza hilo limekuwa sehemu ya maandalizi ya kuelekea mashindano ya SHIMISEMITA yanayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu jijini Mbeya, ambapo halmashauri mbalimbali nchini zitachuana kuwania ubingwa katika michezo tofauti. Akizungumza baada ya bonanza hilo, Afisa Michezo wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Neema Kilongola alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na mechi hizo zimewapa nafasi ya kupima uwezo wa kikosi kabla ya kuelekea Mbeya. “Bonanza hili limetupa nafasi ya kujipima, kurekebisha mapungufu na kuongeza ushindani ndani ya timu. Mwaka jana tulikuwa mabingwa, hivyo mwaka h...

Timu ya Jiji la Dodoma yatakiwa kudumisha nidhamu mashindano ya SHIMISEMITA

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Wachezaji wanaojiandaa kushiriki mashindano ya SHIMISEMITA watakiwa kuwa na malengo makubwa, nidhamu na ari ili kuweza kupata ushindi. Hayo aliyasema Mwenyekiti wa SHIMISEMITA Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Gerald Ruzika wakati wa kikao chake na washiriki wa timu ya Jiji la Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutaho wa halmashauri jijini Dodoma. Aliseama kuwa malengo yetu ni kupambania nafasi ya juu. “Mnakwenda kuiwakilisha Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Muwe na malengo ya ushindi na mkapambane kuurudisha ubingwa kama mlivyofanya mwaka jana. Fanyeni mazoezi kwa bidii, muwe na nidhamu na mshikamano ili mkaandike historia nyingine ya mafanikio,” alisema Dkt. Ruzika. Aidha, aliwasisitiza washiriki kuongeza juhudi katika mazoezi na kuzingatia maelekezo ya makocha wao ili kuhakikisha wanakuwa katika kiwango bora kitakachowawezesha kufanya vizuri na kuipeperusha vema bendera ya Jiji la Dodoma. Kwa upande wake, Nahodha wa Mpira wa Pete, Mwajuma Ban...

Wananchi Kata ya Chang’ombe wahimizwa kulinda miundombinu

Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Wananchi wa Kata ya Chang’ombe watakiwa kuendelea kuitunza na kuilinda miradi ya maendeleo ili iweze kutoa huduma kwa muda mrefu na kuvinufaisha vizazi vya sasa na vijavyo. Hayo aliyasema Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Bakari Fundikira mara baada ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Kata ya Chang’ombe jijini Dodoma. Alisema kuwa serikali imeendelea kuwekeza fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye lengo la kuboresha huduma za kijamii na kuinua ustawi wa wananchi. “Hivyo, ni wajibu wa kila mwananchi kushiriki katika kuilinda na kuitunza. Leo tumetembelea miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Ofisi ya Mtaa wa Kishoka, Ofisi ya Mtaa wa Chang’ombe Juu, Ofisi ya Mtaa wa Hamvu, kisima cha maji Shule ya Msingi Chang’ombe na ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto katika Kituo cha Afya Chang’ombe ambapo miradi hii imejengwa kwa fedha za serikali jumla ya shilingi 456,926,355. Lakini pia nitoe rai kuwa ni m...

Usafi Jumamosi Tarehe 18 Julai, 2026

Image
 

Wataalam Ilemela MC wajifunza mfumo wa utenganishaji taka Dodoma Jiji

  Wataalam kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wamefanya ziara ya mafunzo ya mbinu bora za usimamizi wa usafi wa mazingira hasa mfumo wa kutenganisha taka na kuona vihifadhio vinavyotumika kutenganishia taka katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Ziara hiyo ya mafunzo ilijifunza jinsi kampuni maalum ya kutekeleza miradi (SPV) ya halmashauri inavyotumika kutekeleza miradi ya maendeleo na kutembelea miradi inayotekelezwa ya Bustani ya Mapumziko ya Chinangali na Duka kuuza vifaa vya ujenzi.

Jiji la Dodoma lajinoa kuelekea SHIMISEMITA 2026

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Timu ya Mpira wa Pete ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea kujinoa kuelekea mashindano ya SHIMISEMITA 2026 yanayotarajiwa kufanyika Mwezi Agosti, 2026 jijini Mbeya, mara baada ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Timu ya Jamhuri kabla ya kuingia kwenye dimba la mashindano rasmi. Hayo aliyasema Afisa Michezo wa Jiji la Dodoma, Neema kilongola mara baada ya kutamatika kwa mchezo huo katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma Alisema kuwa michezo ya kirafiki ni sehemu muhimu ya maandalizi kwa kuwa husaidia kubaini mapungufu na kuyafanyia kazi mapungufu hayo. "Lengo la mchezo huu wa kirafiki halikuwa kushinda pekee, bali ilikuwa ni kujipima uwezo wetu, kubaini mapungufu yaliyopo na kuyafanyia kazi kabla ya kuanza mashindano ya SHIMISEMITA. Tunaendelea kujenga timu imara na tunaamini tutafika Mbeya tukiwa katika kiwango kizuri cha ushindani " alisema Kilongola. Aliongeza kuwa kikosi hicho kinaendelea na programu maalum za mazoezi zinazolenga ...

Jiji la Dodoma kinara utekelezaji afua za Lishe

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepata alama ya kijani katika kadi alama ya viashiria vya utekelezaji wa afua za lishe ikiwa ni hatua nzuri kwa kipindi cha Robo ya Nne kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026. Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Lishe kwa kipindi hicho, Kaimu Afisa Lishe wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Happiness Mlamka alisema kuwa utekelezaji umeendelea kufanyika kwa mafanikio makubwa ambapo kadi alama ya lishe imeonesha rangi ya kijani. Alisema kuwa rangi hiyo ni kiashiria kwamba halmashauri imefikia viwango vinavyotakiwa katika utekelezaji wa afua za lishe. Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wake, Sakina Mbugi, aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Dodoma alipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuendelea kufanya vizuri katika utekelezaji wa shughuli za lishe. Alisisitiza umuhimu wa kuendeleza utoaji wa elimu ya lishe kwa kutumia kaulimbiu mbalimbali zinazotolewa kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru, ikiwemo “Zingatia lishe yak...

Wadau wa Lishe watakiwa kuzingatia Sheria

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA Maafisa lishe na watendaji wa kata wametakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utekelezaji wa shughuli za lishe pamoja na kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa afua za lishe. Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa Robo ya Nne ya Mwaka wa Fedha 2025/2026, Sakina Mbugi alipoongoza kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri. “Katika utekelezaji wa shughuli za lishe ni muhimu kuwashirikisha wadau mbalimbali, wakiwemo viongozi wa dini, wazee na vijana, ili kuwapatia uelewa kuhusu umuhimu wa lishe bora. Tunapompa mzee elimu sahihi ya lishe, tunamsaidia kupunguza changamoto za uzeeni na kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza. Hivyo, nitumie nafasi hii kuwaelekeza maafisa lishe na maafisa watendaji wa kata kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utekelezaji majukumu yenu,” alisema Mbugi. Mw...

Jiji la Dodoma latakiwa kushirikisha wadau afua za Lishe

Image
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetakiwa kuongeza ushirikishaji w a makundi mbalimbali ya jamii katika kuimarisha afua za lishe ili kuhakikisha elimu na huduma za lishe bora zinawafikia wananchi wote. Wito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe kwa Robo ya Nne Aprili-Juni, 2026 Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Sakina Mbugi alipoongoza kikao hicho kwa niaba ya mkuu wa wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri. Mbugi ambae ni katibu tawala wilaya ya Dodoma alisema kuwa ni muhimu kuwashirikisha vijana waliopo nje ya mfumo rasmi, wazee, viongozi wa dini, viongozi wa mila, taasisi za serikali na binafsi, watu mashuhuri pamoja na kaya katika kuhamasisha na kutoa elimu ya lishe bora. Ali sema kuwa ushirikishwaji wa makundi mbalimbali ya jamii ni muhimu katika kuongeza uelewa na kuleta matokeo chanya na kubainisha kuwa lishe bora haih usu watoto pekee bali watu wa rika zote. “Sisi, timu ya wataalam, tupo tayar...

RC Senyamule apongeza ujenzi S/M Goba

Image
Na. Mwandishi wetu, MKONZE SHULE ya Msingi Goba iliyogharimu shilingi milioni 302 imeongeza fursa ya upatikanaji wa elimu bora kwa watoto na kuwapunguzia kutembea umbali mrefu kufuata shule katika maeneo mengine. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Msingi Goba iliyopo Mtaa wa Muungano A, Kata ya Mkonze jijini Dodoma. Mkuu wa mkoa aliipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kukamilisha mradi huo unaolenga kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu bora kwa watoto. Vilevile, aliipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa utekelezaji mzuri wa mradi huo na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya elimu ili kukidhi mahitaji yanayotokana na ongezeko la idadi ya watu. “ Nawapongeza kwa kukamilisha ujenzi wa shule hii kwa wakati na kwa viwango vinavyohitajika. Hata hivyo, kutokana na kasi ya ukuaji wa Jiji la Dodoma, ni muhimu kuendelea kujenga miundombinu zaidi ya elimu ili kuhakikisha...

RC Senyamule aridhishwa maendeleo ya ujenzi Jengo Jumuishi Kituo cha Afya Makole

Image
Na. Mwandishi wetu, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepongezwa kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa mradi wa jengo jumuishi la Kituo cha Afya Makole ukitajwa baada ya kukamilika kuwa utaboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi. Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo jana. Mkuu wa mkoa alisema kuwa kukamilika mradi huo kutaleta mapinduzi makubwa katika utoaji wa huduma za afya katika halmashauri. Alisema kuwa jengo hilo linajengwa eneo la kimkakati katikati ya jiji likizungukwa na taasisi za serikali na binafsi. “Jengo hili litapanua huduma ambazo hazikuwepo hapo awali, ikiwemo huduma za dharura, huduma za uzazi na huduma nyingine za kibingwa. Huu ni mradi muhimu ambao utawawanufaisha wananchi wengi. Niwapongeze sana Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa usimamizi mzuri,” alisema Senyamule. Alitumia wakati huo kuwapongeza watumishi wa Kituo cha Afya Makole kwa kuendelea k...

Sekondari Zuzu yapongezwa usimamizi na utunzaji Mazingira

Image
Na. Mwandishi wetu, ZUZU SHULE ya Sekondari Zuzu imepongezwa kwa usimamizi mzuri wa shule na utunzaji wa mazingira jambo linalochochea utulivu wakati wa kufundisha na kujisomea kwa wanafunzi. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alipotembelea na kukagua ujenzi wa mabweni mawili katika Shule ya Sekondari Zuzu. Mkuu wa mkoa alimpongeza Mkuu wa Shule ya Sekondari Zuzu, kwa usimamizi mzuri wa shule hiyo. Alisema kuwa shule ina mazingira safi na rafiki kwa wanafunzi kujifunzia kwa utulivu na walimu kuweza kufundisha vizuri jambo lililopelekea shule hiyo kushika nafasi ya tisa kimkoa miongoni mwa shule za serikali. Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Zuzu, Mwl. Hezron Lupondo aliishukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu kupitia uboreshaji wa miundombinu ya shule. “Ujenzi wa mabweni haya mawili umetupa hamasa kubwa sisi walimu na wanafunzi. Mazingira bora ya kujifunzia yanachangia kuongeza ari ya kufundisha ...

Meya Chaula atembelea banda la Jiji la Dar es Salaam Maonesho ya Sabasaba

Image
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula, ametembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba na kupata maelezo mafupi kuhusu shughuli zinazotekelezwa na halmashauri hiyo.

Wakili Kipangula asisitiza weledi taaluma ya habari

Image
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula ametembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, 2026 yanayoendelea jijini Dar es Salaam na kusaini kitabu cha wageni mara baada ya kupata maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na halmashauri hiyo pamoja na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo jijini Dodoma. Akiwa katika banda hilo aliwataka maafisa habari wa serikali kusimamia misingi ya uandishi wa habari kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma hiyo.

Waziri wa Maendeleo ya Vijana, Joel Arthur Nanauka (Mb) akipokea zawadi kutoka banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba

Image
 

Afisa Biashara Arusha apongeza ukuwaji wa Biashara wa Jiji la Dodoma

Image
Na. Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM   HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepongezwa kwa kasi ya ukuaji wa shughuli za biashara na uwekezaji na kutajwa kuwa ni fursa kwa watanzania na wageni kuwekeza.   Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji Halmashauri ya Jiji la Arusha, John Kilunge alipotembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Kilunge alipongeza kasi ya ukuaji wa shughuli za biashara na uwekezaji ndani ya jiji hilo na kusema kuwa ni fursa kwa watanzania na wageni kuwekeza na kufungua zaidi fursa za ajira. Akiwa katika banda hilo, alipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo, hususan katika sekta za ardhi, biashara na maendeleo ya kiuchumi. Alisema kuwa Jiji la Dodoma linaonesha mafanikio makubwa katika kukuza mazingira ya biashara na kuvutia wawekezaji k...

Jiji la Dodoma lashauriwa kulinda hadhi ya Makao Makuu ya Nchi

Image
Na. Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM   HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeshauriwa kuendelea kusimamia Mpango Kabambe wake ili kuhakikisha jiji linakuwa na mpangilio wa kisasa na kulinda hadhi ya makao makuu ya nchi.   Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Jenifa Omolo (kushoto) akiongea na wataalam wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Jenifa Omolo alipotembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini hapa.   Alisema kuwa ukuaji wa Jiji la Dodoma unapaswa kwenda sambamba na upangaji bora wa maeneo, miundombinu na mazingira ya mji ili kuongeza mvuto zaidi kwa wakazi, wawekezaji na wageni wanaofika kwa shughuli mbalimbali za kiserikali na kiuchumi.   Alisisitiza kuwa taswira ya mji ambao ni makao makuu ya nchi inapaswa kuonekana wazi kupitia mpangilio wa kisasa, unaozing...

Jiji la Dodoma latangaza fursa za Uwekezaji katika Maonesho ya Sabasaba, 2026

Image
Na. Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM Halmashauri ya Jiji la Dodoma imejipanga kujitangaza kama kitovu cha uwekezaji, biashara na maendeleo ya kisasa kutokana na kuwa na fursa nyingi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi jambo linalokuza ustawi wa wananchi na taifa kwa ujumla.   Afisa Habari, Nancy Kivuyo kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma (kulia) akielezea fursa za uwekezaji kwa mdau aliyetembelea banda ya halmashauri  Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Habari katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Nancy Kivuyo alipokuwa akiwaelezea wananchi waliotembelea banda lao jinsi Halmashauri ya Jiji la Dodoma inavyoshiriki katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) mwaka 2026 yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini hapa. Kivuyo alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika kuhakikisha inavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji. “Mazingira ya uwekezaji yameboreshwa sambamba na mazingira ya kufanya...

Maafisa Biashara wa Morogoro na Ruvuma watembelea Banda ya Jiji la Dodoma katika Maonesho ya Sabasaba, 2026

Image
  Na. Mwandishi wetu, DODOMA Maafisa Biashara kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma leo tarehe 1 Julai, 2026 wametembelea Banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.   Wakiwa katika banda hilo, maafisa hao walipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma, ikiwemo ushauri na miongozo kwa wananchi na wawekezaji kuhusu upatikanaji wa maeneo ya uwekezaji na huduma za ardhi, fursa za biashara katika sekta za kimkakati zinazokuwa kwa kasi pamoja na taratibu za uwekezaji ndani ya jiji Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, Mkuu wa Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Lusajo Mwasongwe alisema kuwa wamejifunza mambo mbalimbali yanayoweza kuwasaidia kuboresha utoaji wa huduma katika mamlaka zao. “Tumepata uzoefu mzuri ...