Posts

Showing posts from August 5, 2023

KILIMO CHA ZABIBU 88 DODOMA

 

WAAJIRI DODOMA WATAKIWA KUSAIDIA WANAWAKE KUNYONYESHA WATOTO MAZIWA YA MAMA KAZINI

Image
Na. Dennis Gondwe Dodoma, WAAJIRI katika Mkoa wa Dodoma wametakiwa kutoa msukumo katika kurahisisha na kusaidia wanawake walioajiriwa kuendelea kunyonyesha watoto wao kwa mujibu wa taratibu ili wawe na lishe bora. Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri akiongea na mamia ya wananchi  Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule katika hotuba yake kwenye matembezi ya hiari kuhamasisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama na kusomwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri yaliyoishia uwanja wa Shule ya Msingi Chang’ombe jijini hapa. Senyamule alisema kuwa lengo kuu la maadhimisho ya mwaka huu ni kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kusaidia wanawake waweze kufanya kazi za uzalishaji pamoja na utunzaji wa watoto wao. Alisema kuwa ili kufanikiwa “lazima kuhamasisha na kutetea utekelezaji wa mikakati inayowezesha waajiri kuwa karibu na familia, walezi au mama wa mtoto na kutoa msukumo katika kurahisisha ...

WENZA WA VIONGOZI WASHAURIWA KUANZISHA BUSTANI ZA NYUMBANI

Image
Na. Dennis Gondwe, NZUGUNI WENZA wa viongozi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kuanzisha bustani za nyumbani ili kusaidia familia zao na wageni wanaowatembelea. Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Lucy Kway Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Lucy Kway alipokuwa akiongelea umuhimu wa bustani za nyumbani kwa wenza wa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma alipokuwa akihamasisha kilimo cha bustani hizo kwenye Banda la Jiji la Dodoma katika viwanja vya Nanenane Nzuguni. Kway alisema “nichukue nafasi hii kuwashauri wenza wa viongozi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kulima bustani za nyumbani kwa ajili ya kusaidia familia zao na wageni wanaowatembelea. Hii ni muhimu kwa sababu wenza wa viongozi ni mfano wa kuigwa katika jamii hivyo ni rahisi kwa watu kuiga mfano mzuri kutoka kwa wenza wa viongozi hapa Halmashauri ya Jiji la Dodoma”. Akiongelea kilimo hicho kwa wananchi na watumishi wanaohamia Makao Makuu Do...

CHEMS YAJIKITA KUZALISHA MADUME BORA YA MBUZI DODOMA

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA CHEMS farm imedhamiria kuzalisha madume bora ya Mbuzi aina ya Boha ili kuwasaidia wafugaji kuboresha mifugo yao ya asili katika kanda ya kati. Mfugaji wa Mbuzi kutoka Chems farm, Vendelin Lyakurwa Kauli hiyo ilitolewa na Mfugaji wa Mbuzi kutoka Chems farm, Vendelin Lyakurwa alipokuwa akielezea ufugaji wa Mbuzi katika Banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini hapa. Lyakurwa alisema “lengo la kuzalisha na kuwatunza hawa Mbuzi aina ya Boha ni kuuza madume kwa wenzetu ili waweze kuboresha mifugo yao ya asili. Ukiwa na dume moja kwenye boma unaweza kukusaidia kupata mbegu ambayo wanakua haraka na bei yao ni nzuri na nyama yao ni tamu. Mbuzi hawa ni wa nyama na wanazaa mapacha ukiwalisha vizuri wanazaa pacha watatu mpaka wanne. Wanakuwa haraka wanasoko mpaka uarabuni wanawahitaji hawa Mbuzi. Ni Mbuzi ambao ‘wanaadapt’ mazingira mbalimbali”. Alisema kuwa madume wakitumika kwa Mbuzi wa ki...

JIJI LA DODOMA LAJA NA TEKNOLOJIA YA NISHATI MBADALA MAONESHO YA NANENANE

Image
Na. Dennis Gondwe, DODOMA HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeanzisha teknolojia ya nishati mbadala ili kuondoa matumizi ya kuni na mkaa kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya kati. Afisa Mifugo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, George Joram Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mifugo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, George Joram alipokuwa akiongelea teknolojia ya nishati mbadala inayooneshwa katika banda la mifugo Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Joram alisema “safari hii tumekuja na teknolojia ya nishati mbadala. Tunazalisha gesi kwa kutumia kinyesi cha ng’ombe. Kinyesi cha ng’ombe tunakikusanya kutoka kwenye banda la ng’ombe tunachanganya kwa mchanganyo wa moja kwa moja. Tunachukua kinyesi cha ng’ombe kwenye ndoo ya lita 20 na maji lita 20 tunachanganya na kuzalisha gesi”. Alisema kuwa baada ya saa 24 bacteria wanazalisha gesi inayoitwa Methane. “Badala ya kutumia mkaa na nishati nyingine kama kuni, unaweza kutumia nishati mbadala ya kutumia gesi ya kinyesi cha mifugo na kulinda na ku...