Posts

Showing posts from October 8, 2026

TANESCO wafanya usafi Soko la Machinga Dodoma

Image
  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kwa kushirikiana na maafisa kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Maafisa wa Kanda Namba Moja ya huduma pamoja na wafanyabiashara, wameungana kufanya usafi katika mitaro ya Soko la Wazi la Machinga, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha.   Hatua hiyo inalenga kuhakikisha mitaro inakuwa safi na inapitisha maji kwa ufanisi, hivyo kupunguza athari zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua, huku wafanyabiashara wakihimizwa kuendelea kutunza usafi wa mazingira katika maeneo yao kwa ustawi na usalama wa wote.

Kizota yawekeza zaidi ya Mil. 87 utekelezaji miradi ya maendeleo 2026/2027

Image
Na. Mwandishi wetu, KIZOTA   Kata ya Kizota, jijini Dodoma, imepatiwa fedha kiasi cha shilingi 87,373,170.73 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika mwaka wa fedha 2026/2027, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuboresha huduma za kijamii na miundombinu kwa wananchi.   Akizungumza kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Kizota, Aidani Libenanga alisema kuwa fedha hizo zitatumika katika maeneo mbalimbali yenye umuhimu kwa wananchi, ikiwemo sekta ya elimu, upatikanaji wa maji na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.   Alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 46 kimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, hatua inayolenga kuongeza nafasi za kujifunzia na kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu katika kata hiyo.   Kwa upande wa upatikanaji wa maji, alisema kuwa shilingi 25,073,170.73 zimetengwa kwa ajili ya uchimbaji wa kisima cha maji, ambacho kitasaidia kuongeza upatikanaji wa h...