IAA Tawi la Dodoma kuendelea kulea wataalam kwa vitendo
Na. Alex Sonna, DODOMA CHUO cha Uhasibu Arusha (IAA) – Tawi la Dodoma, kimeendelea kuwa kinara katika kutoa elimu ya vitendo kwa vijana nchini, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2021 kwa kuanza na programu tatu za diploma. Akizungumza katika banda la Chuo hicho katika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima (NaneNane) yanayoendelea katika Uwanja wa Nzuguni, jijini Dodoma, Meneja wa tawi hilo, Dkt. Grace Temba, alisema kuwa chuo hicho ni sehemu ya mtandao wa kitaaluma unaojumuisha kampasi mama iliyopo Dar es Salaam, pamoja na matawi mengine yaliyopo Babati, Songea, Bukombe, Arusha, na Dodoma yenyewe. “Tunapokea wanafunzi kuanzia ngazi ya kidato cha nne ambao husoma kwa miaka mitatu, wakijifunza kupitia mitalaa ya kisasa inayolenga kuwaandaa kwa soko la ajira la sasa na la baadaye,” alisema, Dkt. Temba. Kwa sasa, IAA inatoa jumla ya programu 38 katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na Uhasibu, Usimamizi wa Fedha, Uhasibu wa Kodi, Uongozi na Utawala wa Biashara, Masoko, na Usimamizi wa Ununuz...