Soko la Sabasaba kuongozwa kwa misingi ya uongozi bora
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA Kaimu Mkuu Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Abdul Chacha amewaasa viongozi wa Soko la Sabasaba kuzingatia weledi katika kufanya kazi zao ili kuiishi dhana ya uongozi bora. Aliyasema hayo katika mafunzo waliyoandaa kwa viongozi wa Soko la Sabasaba yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kituo kikuu cha Mabasi Dodoma. Alisema kuwa sifa mojawapo kubwa ya kiongozi bora ni yule mwenye kuzingatia katiba au muongozo wa ushirika ili aweze kutenda haki. “Kiongozi bora ni yule anayejua namna ya kutuimia katiba vizuri. Labda niulize hapa, Katiba ya ushirika ipo? Kama ipo, je ilitumika wakati ule matatizo yameanza kutokea? Jibu litakua hapana. Nipende kuwaambia kuwa, ukiijua vizuri katiba na miongozo, ni rahisi sana Kutenda haki kwasababu utatenda haki kwa kuzingatia taratibu na hakuna atakayelalamika kuwa ameonewa” alisema Chacha. Aliongeza kuwa zipo sifa zaidi ya 25 za kiongozi bora ambapo kila kiongozi wa soko la sabasaba anapaswa ...