Mtoto wa kike apewe fursa ya kuongoza
Na. Faraja Mbise, DODOMA Kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani, ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba 11, jamii imeaswa kumshirikisha mtoto wa kike katika ngazi ya uongozi tangu anapoanza kukua mpaka anapokuwa mtu mzima. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa taasisi ya Msichana Initiatives, Rebecca Gyumi alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Lamaiti, Tarafa ya Mndemu, Wilaya ya Bahi, Mkoa wa Dodoma katika Tamasha la Msichana Amani Music Festival. “Siku hii katika nchi yetu, tunaongozwa na kaulimbiu ya Msichana na Uongozi, Mshirikishe Wakati ni Sasa. Kupitia jukwaa letu la Agenda ya Msichana, tumeitohoa zaidi kaulimbiu yetu ya kitaifa ambapo tunasema Msichana na uongozi, kwakutumia Fursa za Kidijitali au teknolojia ya kidijitali, kwa maana ya kuangalia namna wasichana wanavyoweza kuonesha uongozi kupitia fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye teknolojia ya kidigitali” alisema Gyumi. Wakati akizungumza na kundi la wananchi na watoto wa kike alisema kuwa, ...