Posts

Showing posts from September 3, 2024

Magereza wapongezwa kupambana na ukatili wa kijinsia

Image
Na. Valeria Adam, DODOMA Waziri, Dkt. Gwajima awapongeza wanawake wa Jeshi la Magereza Tanzania kwa kupambana na kuzuia changamoto za ukatili wa kijinsia ili wanawake wachangie katika maendeleo ya taifa. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima akifungua mkutano  mkuu wa kwanza wa Mtandao wa Wanawake wa Jeshi la Magereza Tanzania Pongezi hizo zilitolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa kwanza wa Mtandao wa Wanawake wa Jeshi la Magereza Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Mtakatifu Peter jijini Dodoma. “Hatua hii inaonesha ni jinsi gani sera na miongozo mbalimbali ambayo serikali inatoa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia katika maeneo mbalimbali nchini, inavyotekelezwa kwa vitendo. Na ninyi mmegeuza miongozo na sera kuwa vitendo kwa kuratibu nchi nzima wanawake katika jeshi hili la Magereza. Utekelezaji huu ambao umenigusa pia ni kwa saba...