Posts

Showing posts from September 16, 2026

Zoezi la Kuua Mbwa Wanao Zurura Lafanyika Kata ya Msalato

Image
Na. Manase Malima, MSALATO   Zoezi la kuua mbwa wanao zurura limefanyika katika Kata ya Msalato, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, likihusisha maeneo ya Machinjioni, Magereza na Mnadani, kutokana na kero na hatari zinazowakabili wananchi ambapo mbwa zaidi ya 20 waliuliwa. Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Afisa Mifugo wa Kanda Namba Sita ya utoaji huduma Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prisca Mottee alisema kuwa mbwa hao wamekuwa wakisababisha usumbufu kwa wananchi, wakiwemo watoto na wanafunzi wanaokwenda na kurudi shuleni, Afisa Mifugo kanda Namba Sita aliongeza kuwa zoezi hilo ni endelevu na litafanyika katika maeneo mengine yenye changamoto hiyo, huku akiwataka wafugaji kuwafungia mbwa wao na kuzingatia kuwapatia chanjo. Kwa upande wake Afisa Mifugo Kata ya Msalato, Maisha Jiwa alisema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kufuatia malalamiko ya wananchi kuhusu mbwa wanao zurura katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo. “Kumekuwa na adha kubwa ya mbwa wanaozurura katika maeneo ya Machi...