Posts

Showing posts from March 1, 2025

Wananchi waanza ujenzi sekondari ya Kata ya Chahwa jijini Dodoma

Image
Na. Nancy Kivuyo, CHAHWA Mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kata ya Chahwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamefanikiwa kuzindua utekelezaji wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari kwa nguvu zao wenyewe kwa lengo la kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi. Akizungumza na wananchi hao, Diwani wa Kata ya Chahwa, Sospeter Mazengo aliwapongeza wananchi kwa moyo wa utayari na michango katika kujenga shule ya sekondari itakayopunguza adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kupata huduma ya elimu. Baadhi ya wananchi walichanga pesa taslimu pamoja na vifaa vya ujenzi, alisema. ā€œWatoto wetu wamekua wakiteseka kutembea umbali mrefu kutoka Chahwa hadi Ipala kusoma, ninaamini tutafanikiwa katika hili tuliloazimia kulifanya kama tutaanza kwa nguvu ya pamoja. Inawezekana baadae kupata wadau wakatusaidia kumalizia pale ambapo tutaishiaā€ alisema Diwani Mazengo. Sambamba na hilo, aliwasisitiza kuwa kupitia maazimio yao waliyojiwekea kufikia mwezi Januari, 2026 madarasa manne yawe yamekamilika na masomo...