Posts

Showing posts from March 2, 2025

Wanafunzi Hazina Sec watakiwa kufunguka dhidi ya ukatili

Na. Halima Majidi, HAZINA Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Hazina, iliopo katika Kata ya Hazina, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, wametakiwa kuwa wawazi na wakweli katika kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia ili kuepuka vitendo hatarishi vitakavyo sababisha kudumaza fikra na ufaulu katika masomo yao. Hayo yalisemwa na Afisa Mtendeji wa Kata ya Hazina, Tunu Dachi alipofanya ziara ya utoaji wa elimu juu ya masuala mbalimbali katika kata hiyo. Alisema kuwa inabidi ziara zifanyike mara kwa mara za kutoa elimu ili watoto wetu waweze kujitambua waelewe majukumu yao wakiwa shuleni, waweze kusoma katika mazingira mazuri kiakili na kihisia. ā€œLeo tumekuja shuleni kama 'normal routine' kwaajili ya kuwatembelea watoto, kuwapa elimu dhidi ya ukatili kwa ujumla, watoto wamekuwa wakweli wameuliza maswali ambayo sisi yametupa kazi ya kwenda kuyafanyia kazi na kuwaletea majibu chanyaā€™ alisema Dachi. Alisema kuwa, anaamini ili mwanafunzi afanye vizuri sio mpaka awe na majengo na walimu waz...