Posts

Showing posts from January 14, 2025

Kambi: Watoto wenye mahitaji maalum wanahaki ya kusoma

Image
Na. Coletha Charles, CHANG’OMBE Kata ya Chang’ombe, Halmashauri ya Jiji la Dodoma imebainisha na kuwaandikisha watoto wenye mahitaji maalum kwa lengo la kujiunga na elimu ya awali na msingi kwa mwaka wa masomo 2025 kwa kushirikiana na wazazi, walezi na walimu.   Afisa Elimu Maalum Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Issa Kambi akifanya uchunguzi mwanafunzi mwenye mahitaji maalum Akizungumza wakati wa uandikishaji wa watoto hao, Afisa Elimu Maalum Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Issa Kambi, alisisitiza kuwa jukumu la kuwapatia watoto hao fursa ya kusoma lipo mikononi mwa wazazi na walezi kwa sababu wanahaki ya kupata elimu kama watoto wengine kwa kuwajengea msingi bora wa maendeleo.   Alisema kuwa, serikali imejipanga kuwahudumia watoto wenye mahitaji maluum kwa kuwapokea na kuwapa mahitaji stahiki na kuhakikisha wanapata nafasi bila kujali changamoto zao. “Wazazi ukiwa na mtoto usichoke kumlea, ukiona umechoka basi huyo mtoto amefanikiwa na tusiwakatie tamaa. Watot...