Shilingi Bilioni 1.5 kujenga Hospitali ya Wilaya Dodoma
Na. Dennis Gondwe, DODOMA SERIKALI imetoa shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Dodoma katika jitihada za kusogeza huduma bora za afya karibu zaidi na wananchi. Moja ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Dodoma Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Andrew Method alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha miaka mitatu kwa waandishi wa habari ofisini kwake jijini hapa. Dkt. Method alisema “tunapoongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha miaka mitatu, mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Dodoma. Na hiyo hospitali ya wilaya ipo kimkakati kabisa, inajengwa eneo la Kata ya Nala. Ni eneo ambalo linaweza kufikiwa na rufaa ya vituo vyote vya afya ambavyo vinapitiwa na barabara ya mzunguko ‘ring road’. Kwa hiyo utaona hii barabara ya mzunguko inae...