Maboresho ya elimu yapelekea kuongezeka kwa ufaulu katika Shule za Awali na Msingi Dodoma
Na. Nancy Kivuyo, KIWANJA CHA NDEGE Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Halmashauri ya Jiji la Dodoma yafafanua mafanikio ya maboresho ya elimu katika shule za msingi ambayo inafanya ufaulu wa wanafunzi kuongezeka. Ufafanuzi huo ulitolewa katika Mkutano wa Wadau wa Elimu na Utambulisho wa Mfuko wa Chakula na Lishe Shuleni ikiwa ni sehemu ya kujadili suala la lishe bora kuboreshwa kwa asilimia zote ili taaluma ya wanafunzi ifikie lengo tarajiwa. Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Prisca Myalla alisema ātunaishukuru serikali yetu kupitia Ofisi ya Rais ā TAMISEMI kwa kuboresha elimu na kujenga miundombinu mizuri ambayo kwasasa inasaidia utoaji wa elimu kuwa mzuri. Katika suala la lishe, tunashukuru mfuko wa chakula na lishe shuleni kwasababu unasaidia wanafunzi kuhudhuria shuleni hali inayopelekea mahudhurio kuwa juu ukilinganisha na kipindi cha nyumaā. Akizungumza kuhusu hali ya ufaulu na jumla ya s...