Wafanyabiashara kuboresha huduma na kukuza biashara Mwaka 2025
Na. Halima Majid na Shahanazi Subeti, DODOMA Wafanyabiashara waweka wazi malengo ya kuboresha huduma ya kukuza biashara zao na kuchangia maendeleo ya uchumi ya Jiji la Dodoma mwaka 2025. Hayo yalisemwa na wafanyabiashara wa eneo la One Way lililopo katikati ya Jiji la Dodoma wakati wa mahojiano na waandishi wa habari walipokuwa wanaelezea salamu za jinsi walivyoupokea mwaka mpya 2025. Mfanyabiashara wa urembo, Luqman Olomi, katika Mtaa wa One Way alisema changamoto kubwa ni matatizo ya kifamilia yanayopelekea kurudishwa nyuma kiuchumi na kusababisha biashara yake kuyumba kwa kiasi flani. "Kuna changamoto za kifamilia zaidi ambazo huwa zinaturudisha nyuma kwa kiasi kikubwa kwa sababu inabidi utumie mpaka kiasi ambacho umeweka kwa ajili ya biashara na ili tufanikiwe inatakiwa tujitegemee na tusitegemee cha mtu. Hiyo ndio siri ya mafanikio na kwa anayoyafanya Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na mashirika mengi na taasisi mbalimbali anafanya vizuri” alis...